RC Tabora aagiza kukamatwa kwa viongozi wa ushirika..
Serikali ya Mkoa wa Tabora imeagiza kukamatwa kwa waliokuwa viongozi wa Chama cha Ushirika cha Mibono na wale Tupendane kwa ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za wakulima na vyama hivyo. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wa hadhara ambao ni sehemu ya utekelezaji wa magizo ya viongozi wakuu wa kitaifa wa kuagiza kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi. Amesema kuwa viongozi wote wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za vyama na wakulima na wale wakulima wa tumbaku waliotorosha tumbaku katika msimu wa 2013/14 watafutwe popote walipo na kukamatwa ili waweze kufikishwa Mahakamani. Mwanri amesema kuwa hata kama kuna kiongozi yoyote aliyehusika na ambaye amehama ni vyema akarudishwa ili hatua za kisheria dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za AMCOS. “Nakuagiza DC shirikiane na OCD mkitumia taarifa ya ukaguzi wa vyama vya msingi hivyo fedha za wakulima kisha muwakamate na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili wapate adhab