Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2014

CHAWAUMAVITA kuaadhimisha siku ya CP Duniani.

Na GEOFREY ESTON CHAMA cha Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA),kitafanya maadhizimisho ya siku ya CP Duniani katika Viwanja vya Mnazi mmoja oktoba 2 mwaka huu Jijini Dar es salaam. Kikiwa  na lengo la kusaidiana na Taasisi nyingine kwa kupunguza changamoto zinazowakabili watoto wenye Ulemavu na kutafuta njia za kuwasaidia watoto hao, maadhimisho ya siku ya CP Duniani hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni mwendelezo wa mwaka jana "CHANGE MY WORLD IN ONE MINUTE". Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Jonathan Kawamala, ameeleza Dira ya chama chao ni kuchangia upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,akili na Viungo Tanzania ili kuhakikisha watoto wenye ulemevu wa Mtindio wa Ubongo akili na viungo wanasaidiwa kukabiliana na changamoto zilizopo na kuandaa mazingira bora ya makuzi na maisha yao kwa ujumla. Kawamala alisema katika maadhimisho ya mwaka huu...

Daktari mwengine wa Ebola aaga dunia

Picha
Ebola Ripoti kutoka Sierra Leone zinasema kuwa daktari mwengine amefariki kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola. Afisa huyo aliambukizwa ugonjwa huo wakati alipokuwa akiwatibu wagonjwa wa Ebola. Zaidi ya maafisa 20 wa afya wameaga dunia katika taifa hilo huku wengine wengi wakifanya mgomo wakidai marupurupu yao. Awali ,liberia ili-ufungua mtaa mmoja wa mabanda uliokuwa umetengwa kwa kipindi cha juma moja ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo. Zaidi ya watu 1500 wamepoteza maisha yao magharibi mwa Afrika kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huo hatari mnamo mwezi Machi. Source:BBC Swahili

Lead Story za leo mwisho wa mwezi wa August 31,2014 katika magazeti ya hapa nchini.

Picha
Source:MillardAyo.com

Loic Remy kujiunga rasmi na klabu ya Chelsea ya nchini uingereza.

Picha
Baada ya Fernando Torres kukamilisha usajiri wake wa mkopo wa miaka miwili katika klabu ya AC Milan akitokea katika klabu ya Chelsea,Loic Remy amekuwa mbadala wake katika nafasi ya ushambuliaji wakisaidiana na washambuliaji wenzake kama Didier Drogba na Diego Costa katika klabu hiyo ya Chelsea. Remy ambaye ni mshmbuliaji wa timu ya taifa ya ufaransa na alikuwa akichezea katika klabu ya QPR ya hapo Uingereza na kuhamia rasmi Chelsea kwa ada ya uhamisho paundi millioni 10. Ukumbuke Remy alifeli vipimo vya afya alipokuwa akikaribia kujiunga na Liverpool mwanzoni mwa dirisha la usajili.

Na hii ndio video mpya ya P-square ft T.I inayoitwa Ejeajo

Lead Story za leo tarehe 30.2014 za magazeti mbalimbali ya hapa nchini.

Picha
Source:Millard Ayo.com