Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2014

CHAWAUMAVITA kuaadhimisha siku ya CP Duniani.

Na GEOFREY ESTON CHAMA cha Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA),kitafanya maadhizimisho ya siku ya CP Duniani katika Viwanja vya Mnazi mmoja oktoba 2 mwaka huu Jijini Dar es salaam. Kikiwa  na lengo la kusaidiana na Taasisi nyingine kwa kupunguza changamoto zinazowakabili watoto wenye Ulemavu na kutafuta njia za kuwasaidia watoto hao, maadhimisho ya siku ya CP Duniani hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni mwendelezo wa mwaka jana "CHANGE MY WORLD IN ONE MINUTE". Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Jonathan Kawamala, ameeleza Dira ya chama chao ni kuchangia upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,akili na Viungo Tanzania ili kuhakikisha watoto wenye ulemevu wa Mtindio wa Ubongo akili na viungo wanasaidiwa kukabiliana na changamoto zilizopo na kuandaa mazingira bora ya makuzi na maisha yao kwa ujumla. Kawamala alisema katika maadhimisho ya mwaka huu...