Tume ya Uchaguzi Tanzania yasema iko tayari..
Jaji Damian Lubuva. Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imekutana na wamiliki wa vyombo vya habari Jumatano na kuwapa muhtasari wa maandalizi ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu Katika mkutano huo mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva ameeleza kwamba kwa kiasi kikubwa maandalizi ya uchaguzi mkuu yamekamilika ambapo sasa wako katika mchakato wa mwisho wa kuchapisha daftari la wapiga kura baada ya kuweka hadharani lile la awali huku vifaa vingine vya uchaguzi vikiwa vimekamilika kwa asilimia kubwa. Naye Kaimu mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi Emmanuel Kawishe aliwahakikishia wamiliki wa vyombo vya habari juu ya kuwepo na umakini wa kutosha katika uhakiki wa kura mara baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika Tume ya taifa ya uchaguzi pia ilizungumzia kuahirishwa kwa chaguzi mbili za ubunge katika majimbo mawili ambayo baadhi ya vyama vimepoteza wagombea wao kwa kufariki dunia, katika majimbo ya Lushoto kwa CHADEMA na...