Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2016

Ratiba Ligi kuu Tanzania Bara Azam na Simba hapatoshi wikiend hii..

Picha
Mechi za VPL zina tarajia kuendelea wikiend hii kwa mechi mbali mbali huu ukiwa ni muda wa lala salama wa Ligi Kuu na kila timu kati ya tatu za juu inatafuta kushinda mechi zote, itakuwaje Jumapili kati ya Simba na Azam na huko Mwanza Yanga atakuwa mgeni wa timu ya Toto Africans ambayo inapambana isishuke daraja. Hii ndo ratiba za Mechi wikiendi hii Toto Africans vs Young Africans 30-04-2016 African Sports vs Coastal Union 30-04-2016 Mwadui FC vs Stand United 30-04-2016 Mtibwa Sugar vs Mbeya City 30-04-2016 Tanzania Prisons vs JKT Ruvu 30-04-2016 Simba SC vs Azam FC 01-05-2016 Source:Bongo 5

Dubai kwenye mpango mpya utakaovunja rekodi ya dunia..(+Pichaz)

Picha
Dubai  ni mji ambao kwa sasa watanzania wengi wanaenda kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali,  Dubai   umekua kwa haraka zaidi kutokana na kuweka vizuri njia za ukusanyaji wa mapato na ni mfano ya mji ambao Uongozi wake unafanya kazi kwa kuwa baada ya miaka 25 macho ya Dunia nzima yamehamia  Dubai. Dubai wameelezea mipango yao zaidi kwenye mji huo ambapo maeneo ya makazi mapya, Dubai Creek Harbour yatauzunguka mjengo mrefu ambao bado haujapatiwa jina lakini nickname yake ni ‘ the needle ‘. Mjengo huo utakuwa mrefu kuzidi uliopo wa  Burj Khalifa   wenye 2,717 ft na umepangwa kujengwa 2020. Source:Millardayo.com

Magufuli: Polisi sharti wajirekebishe..

Picha
Rais Magufuli amesema baadhi ya mambo yanachangia kuwepo kwa hali ngumu ya utendaji kazi. Rais wa wa Tanzania Dkt John Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini pamoja na ofisi ya mwendesha mashitaka kujirekebisha katika utenda kazi na kujiepusha na kashfa. Amesema taarifa zinaonesha jeshi la polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi. Akiongea alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, Dodoma ametoa mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari. Aidha, amezungumzia mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya polisi na wawekezaji akisema baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo. “Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka muele...

TCRA yazindua nyimbo maalum ya uhamasishaji kwa wananchi kuhakiki simu zao za mkononi.

Picha
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania imezindua wimbo maalum wa kuhamasisha wananchi kuhakiki simu zao wakati wa kuelekea ukomo wa matumizi ifikapo tarehe 16 Juni 2016. Akiongea na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Mhandisi James Kilaba amesema licha ya mamlaka ya mawasiliano kusimamia kwa karibu makampuni ya simu hapa nchini katika uendeshaji wa kila siku wa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha simu yake imehakikiwa ili kuzuia usumbufu wowote utakao jitokeza wa kipindi cha mpito kitakapo malizika mwezi Juni.   Katika hatua nyingine kaimu mkurugenzi huyo alimtambulisha mtunzi wa nyimbo maalum kwaajili ya uhamasishaji wa uhakiki ambaye ni msaanii wa muziki kutoka Tanzania House of Talent (THT) Bwana Hammad Hassan ambaye alielezea kuguswa na zoezi hilo.   Kwa upande wao wananchi waiomba serikali kuendelea kutoa elimu zaidi ili waweze kujua ni jinsi gani wanaweza kuhakik...

Liverpool yachapwa Europa League..

Picha
Liverpool walichapwa 1-0 Mechi za kwanza za nusu fainali za Uefa Europa League zimechezwa jana, mabingwa watetezi Sevilla wakicheza ugenini na Shakhtar Donetsk. Matokeo ya mchezo huo ni kwamba Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo. Sevilla ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 6 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Mchin Perez, na Shakhtar Donetsk kusawazisha bao hilo dakika ya 23 kupitia kwa Maros Romeo na Stepanenko kuongeza bao la pili dakika ya 35 kipindi cha kwanza. Baadaye kelvin Gameiro akaisawazishia Shakhtar Donetsk ikasawazisha bao hilo dakika ya 82 kwa njia ya penati . Katika mchezo mwingine Klabu ya England Liverpool ikicheza Ugenini huko Uhispania imeambulia kichapo cha bao 1-0 mikononi mwa Villarreal kwa bao la Adrian Lopez la dakika ya 90 ya mchezo. Timu zote nne zitarejeana tena Alhamisi wiki ijayo, ikiwa ni mechi za pili hatua ya nusu fainali. Source:BBC ...

Wenger:Arsenal ilipoteza taji la ligi nyumbani..

Picha
Arsene Wenger Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa timu yake ilipoteza harakati za kushinda ligi wakati wa kucheza mechi za nyumbani dhidi ya timu zilizo chini ye jedwali. Arsenal iliopo katika nafasi ya nne imeshinda mechi sita kati ya mechi 16 ilizocheza. Baadhi ya mashabiki wamemtaka raia huyo wa Ufaransa kuondoka katika mechi za hivi karibuni. Ni lazima tujue kwamba ugenini tumekuwa washindi . Arsenal Lakini nyumbani dhidi ya timu ndogo tulipoteza pointi nyingi,alisema Wenger. Maandamano zaidi yanatarajiwa wakati wa mechi ya Jumamosi katika uwanja wa Emirates dhidi ya Norwich. Source:BBC