Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2016

Boko haram yauwa wanajeshi 34 Niger..

Picha
Rais wa Niger Mahamadou Issoufou Shambulizi hilo lilizuka jumamosi mchana wakati ambapo maelfu ya wapiganaji wa Boko Haram walipoelekea Bosso na kuchukua magari yaliyokuwa na silaha nzito. Kundi la wanamgambo la Boko Haram limeshambulia kusinimashariki mwa Niger na kuuwa wanajeshi 34 na kujeruhi wengine 67. Shambulizi hilo lilizuka jumamosi mchana wakati ambapo maelfu ya wapiganaji wa Boko Haram walipoelekea Bosso na kuchukua magari yaliyokuwa na silaha nzito. Wapiganaji hao wa Boko Haram walitumia silaha nzito hata kabla ya kuingia kwenye mji huo . Wanajeshi wa Nigeria walilazimishwa kuondoka katika kambi yao kilomita 20 mbali na mji ili kujiandaa kusaidia. Vikosi vya ulinzi na usalama baadae vilichukua tena udhibiti wa mji . wanajeshi wawili wa Nigeria ni miongoni mwa waliouwawa. Washambuliaji waliweza kuchukua magari yenye silaha nzito na vifaa vingine . hivi sasa watu bado wanaishi katika hali ya wasiwasi kufuatia shambulizi hilo, ingawa mji uko kimya. ...

Mwandishi wa habari wa kike auawa Somalia..

Picha
Mwanamke mmoja mwandishi wa habari ameuawa kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Sagal Salaad Osman, ambaye alikuwa akifanya kazi na kituo cha serikali aliuawa na watu waliokuwa wamejihami na bastola. Somalia ni moja ya nchi hatari zaidi duniani kwa waandishi wa habari, lakini kuuawa kwa waandishi wa habari wa kike si jambo la kawaida. Hakuna kundi lililodai kutekeleza mauaji hayo, lakini huenda yametekelezwa na kundi la al Shabaab ambalo mara nyingi huwalenga waandishi wa habari. Source:BBC

Guinea Bissau na Ghana zafuzu kwa kombe la Afrika..

Picha
Kikosi cha Guinea Bissau. Guinea Bissau ikefuzu kwa kombe la taifa bingwa abarani Afrika kwa mara ya kwanza kabisa. Bada ya kuwashinda Zambia siku Jumamosi, nafasi yao katika kinyanganyiro hicho cha mwaka ujao ilidhihirika wakati Congo-Brazzaville walipoteza kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Kenya. Ghana ilifaulu kufuzu baada ya kushinda ugenini kwa mabao mawili wa bila dhidi ya Mauritius. Source:BBC

Seriakali yadaiwa sh6 trilioni..

Picha
Jengo la PPF House, jijini Dar es Salaa Kamati ya Bajeti imesema moja ya eneo ambalo Serikali ina changamoto kubwa ya kutatua  madeni yake ni katika  mifuko ya jamii yanayofikia zaidi ya Sh6 trilioni. Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo makamu mwenyekiti Josephat Kandege amesema licha ya Serikali kuonyesha nia njema ya kulipa madeni hayo likiwamo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF bado utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua. “Mfano kwa mwaka wa fedha 2015/16, Serikali iliahidi kutoa kiasi cha Sh150 bilioni pamoja na kutoa Non Cash Bond ya Sh2.6 trilioni ili kulipa deni la PSPF lakini hadi sasa ni Sh83 bilioni tu zilizotolewa na hakuna Non Cash Bond yoyote iliyotolewa,”amesema Kandege. Amesema kuwa kamati inaona madeni hayo ni tishio kubwa linaloathiri utekelezaji wa majukumu ya mifuko husika hasa ulipaji wa pensheni ya wastaafu wanaongezeka kila mwaka. Source:Mwananchi ...

Mabondia wa kulipwa ruksa kushiriki kwenye Olimpiki mwaka huu..

Picha
Mabondia wa kulipwa akiwemo Floyd Mayweather wanaweza kushiriki kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu Mabondia wa kulipwa wameruhusiwa kushiriki kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu jijini Rio de Janeiro, Brazil baada ya chama cha ndondi cha kimataifa, AIBA kukubali kubadilika kwa katiba, Jumatano hii. Rais wa AIBA, Ching-Kuo Wu alisema kubadilika kwa katiba ya AIBA kumepitishwa kwa asilimia 95 na wajumbe 84 kati ya 88. Hiyo inamaanisha kuwa mabondia wa kulipwa sasa wataweza kuwania medali kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo yanayoanza Aug. 5. Jumla ya mabondia 286 watashiriki kwenye mashindano hayo. Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Mike Tyson, aliyewahi kushinda medali ya dhahabu kipindi anacheza ngumi za ridhaa mwaka 1981 na 1982 kwenye Junior Olympic Games, ameikosoa hatua hiyo. “It’s ridiculous, it’s foolish, and some of the pro fighters are going to get beat by the amateurs. It’s just going to happen, I really believe that,” bondia huyo aliliambia shiri...

HII HAPA RATIBA KAMILI YA ZIARA YA KIMICHEZO YA MBEYA CITY NCHINI MALAWI..

Picha
Siku chache baada ya kumalizika kwa Ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015/16, Ratiba ya mwanzo ya michezo kadhaa ya kirafiki ambayo kikosi cha Mbeya City Fc  kitacheza kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya wa 2016/17 imetoka. Kwenye ratiba hiyo, City imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka dimbani Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18 kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets, ambapo kwa mujibu wa waandaaji, mchezo unatarajia kushuhudiwa na watazamaji wengi hasa ukizingatia ushawishi wa timu hiyo kwenye soka la nchi hiyo. Mkuu kitengo cha habari na mawasiliano kwenye kikosi cha City,  Dismas Ten  , amesema kuwa mchezo wa pili nchini humo utachezwa jijini Lilongwe na utakuwa dhidi ya wenyeji Civo United, kwenye dimba la Civo Stadium hii itakuwa ni Juni 21. “Baada ya mchezo huo wa pili jijini Lilongwe, tutarudi kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi hiyo, Mzuzu, hapo tutacheza na wenyeji wetu Mzuni Fc, Juni 25 hu...

Garissa university attack plotter Mohamed Kuno 'dead'...

Picha
Mohamed Kuno was a headmaster in a school in Garissa before attacking the town The leader of the attack on Garissa University in Kenya has been killed, officials in Somalia say. Kenya's government said Mohamed Kuno was behind the attack in April 2015 that killed 148 people. Regional forces in Somalia said he was one of 16 people killed in an overnight raid on their convoy in Kismayo, a port city in southern Somalia. Four of those who died were reportedly senior members of the al-Shabab Islamist militant group. The BBC's Africa security correspondent, Tomi Oladipo, said the news comes as a huge boost for Somalia and its allies in the fight against al-Shabab. However, at least 10 people were killed on Wednesday by a car bomb outside a hotel in Somalia's capital Mogadishu, that was claimed by al-Shabab. The news of Kuno's death was confirmed in a press conference held by Abdirashid Janan, the security minister in the Somali region of Jubaland. Who wa...

Uturuki yafungua Ubalozi Kigali..

Picha
Kigali, Rwanda Kwa mara ya kwanza, Uturuki imefungua ubalozi wake mjini Kigali.Serikali ya Rwanda imekaribisha uamuzi huo wa Uturuki na kusema kuwa unaondoa adha iliyokuwepo ambapo wananchi wa Rwanda waliotaka kusafiri Uturuki walilazimika kwenda Kampala, Uganda kuomba visa ya kusafiria. Uamuzi huo umefuatia ule wa Rwanda wa kufungua ubalozi wake mjini Ankara Uturuki miaka 4 iliyopita. Nchi zote mbili zimesaini mikataba mbali mbali ya ushirikiano na maendeleo . Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki amesema mikataba hiyo inalenga kuinua kiwango cha uwekezaji baina ya mataifa yote mawili. Kama anvyosimulia Sylvanus Karemera kutoka Kigali. Source:VOA