Machapisho

Nigeria:Watu 29 wauawa msikitini

Picha
Watu 29 wameuawa katika mji wa Maiduguri Watu 29 wameuawa kati mji mkuu wa jimbo la Borno Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua ndani ya msikiti. Kamishna wa polisi katika jimbo la Borno amesema kuwa watu wengine 28 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo. Shambulizi hilo lilifuatia jaribio la awali la kuuteka ya mji wa Maiduguri lililondeshwa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram. Wanagamabo hao walifyatua makombora kwenye makazi ya watu na kuua takriban watu 13. Rais Buhari ameapa kukabiliana kikamilifu na wapiganaji wa Boko Haram Siku ya ijumaa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari aliahidi wakati wa kuapishwa kwake kuwa atakabiliana vilivyo na kundi hilo la wapiganaji wa Boko Haram. Rais Buhari alisema kuwa kituo cha kijeshi kitawekwa katika mji wa Maiduguri kusadia kupigana na wanamgambo hao. Rais Buhari akihutubia taifa punde baada ya kuapishwa alisema kuwa jeshi la taifa hilo litakita kambi yake katika mji huo wa...

Dk Bilal amezindua chuo kikuu kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo akisistiza uwekezaji katika elimu ya sayansi kwa vijana.

Picha
Makamu wa rais Dk Mohamed Gharb Bilali amezindua chuo kikuu kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo mkoani Pwani akisistiza uwekezaji katika elimu ya sayansi kwa vijana kama hatua ya dira kusimamia vyema rasilimali za nchi ikiwemo madini, mafuta na gesi. Makamu wa rais Dk. Gharibu Bilali katika kusistizaelimu ya sayansi amesema serikali itaendelea kufungua fulasa kwa watanzania na asasi mashirika ya dini ili kuwekeza katika elimu husisansa na tehama kama hatua ya kukidhi mahitaji na ushindani wa soko la ajira duniani na kuliepusha taifa kuendelea kutumia wataalam kutoka nje ya nchi.   Uzinduzi huo ulitanguliwa na ibada maalumu iliyongozwa na askofu kanisa katoliki mkuu jimbo la Morogoro Mhasham Telesphori Mkude ambaye katika kunukuu vitabu vitakatifu amewataka watanzania kujiepusha na watu wenye uchu wa madaraka pamoja na mafisadi wanaoweza kuliangamiza taifa hususan wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu octoba mwaka huu.   Awali makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu ...

Maandamano yafanyika Venezuela

Picha
Waandamanaji Venezuela Maelfu ya watu wamefanya maandamano ya amani nchini Venezuela wakipitia barabara za mji mkuu Caracas wakitaka kuachiliwa kwa viongozi wa upinzani ambao wamekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja. Wanasiasa hao ni pamoja na mameya wawili wa zamani Leopoldo Lopez na Daniel Ceballos ambao wanazuiliwa kwa mashtaka ya kuchochea maandamano ya kuipinga serikali. Rais wa Venezuela Nicholas Maduro amewalaumu kwa vifo 43 vilivyotokea wakati huo. Wiki hii wawili hao walitangaza kuanza mgomo wa kutokula wakiwa gerezani. Source(Bbc Swahili)

Magazeti ya leo Jumapili, tarehe 31.5.2015 na Vichwa mbalimbali vya magazeti...

Picha

Waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ametangaza rasmi nia ya kuwania urais wa kupitia chama cha mapinduzi CCM.

Picha
Mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ametangaza rasmi nia ya kuwania urais wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi mbele ya umati wa watu waliofurika uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha na kutaja vipaumbele vyake kuwa ni elimu,kupambana na umaskini,kulinda rasilimali za nchi  na kuwaunganisha watanzania . Mh.Lowassa ambaye aliingia.uwanjani akisindikizwa na msafara wa pikipiki na magari pia  amesema akipewa fursa atahakikisha  anadumisha muungano.   Amesema ataweka misingi imara ya kuharakisha maendeleo mazuri kwa wananchi  na kuwawezesha vijana kuondoa tabaka la walionacho nawasionacho.   Awali viongozi wa dini na siasa akiwemo Kkingunge Ngombale Mmwiru wameseama Lowassa ana sifa za kiongozi anayefaa kuliongoza  taifa  kwa sasa.   Sherehe hizo zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka kona mblimbli  nchini burudani kubwa  ilikuwa  ni  Helkopta ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa G...

ARSENAL YATWAA KOMBE LA FA KWA KUICHAPA ASTON VILLA 4-0

Picha
Mabingwa mara 12 wa Kombe la FA, Arsenal baada ya ushindi wa jana dhidi ya Aston Villa. Arsenal wakisherehekea ubingwa wao wa FA. Theo Walcott akiifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 40. Walcott akishangilia bao hilo. Alexis Sanchez (kushoto) akipiga shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Arsenal bao la pili. Per Mertesacker akipiga mpira wa kichwa uliozaa bao la tatu kwa Arsenal. Olivier Giroud akifanya hitimisho kwa kutupia kambani bao la nne. ARSENAL imetwaa Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika fainali iliyopigwa katika Uwanja wa Wembley usiku huu. Mabao ya ushindi ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika ya 40, Alexis Sanchez dakika ya 50, Per Mertesacker dakika ya 61 na Olivier Giroud aliyeingia kipindi cha pili na kufunga bao dakika ya 90. Kwa matokeo ya jana, Arsenal wameweka rekodi ya kulichukua kombe hilo mara nyingi kuliko timu nyingine yoyote wakiwa wameli...

China yatetea miradi yake baharini

Picha
Su Jianguo - Naibu mkuu wa majeshi nchini China Mmoja wa makamanda wa ngazi za juu katika jeshi la China ametetea sera za China za kujenga miradi katika maeneo yanayozozaniwa baharini katika bahari ya kusini mwa china siku moja baada ya marekani kutaka miradi hiyo kusitishwa mara moja. Su Jianguo ambaye ni naibu wa mkuu wa majeshi aliuambia mkutano mkuu nchini singapore kuwa miradi hiyo ina lengo la kuboresha uwezo wa China wa kutekeleza majukumu yake ya kimataifa na kusaidia eneo hilo. Alisema kuwa kati ya majukumu hayo ni pamoja na jitihada za uokoaji, utunzi wa mazingira na uhuru wa safari za baharini. China inasema kuwa karibu eneo lote la kusini mwa bahari ya china ni lake. Source(Bbc Swahili)