Machapisho

Kilichojadiliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA leo, kuja na tamko hili Jumatatu..

Picha
Kesho Jumatatu July 31, 2017 Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kitakutana na  Waandishi wa Habari Dar es Salaam kutoa tamko juu ya maazimio na hutua zitakazochukuliwa na Chama hicho kuhusiana na mambo mbalimbali. Hatua hiyo inakuja baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho kukutana kwa siku mbili mfululizo July 29-30, 2017 katika Hotel ya Double Tree, Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda zao. Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema imesema kuwa ajenda ambazo zimejadiliwa ni pamoja na hali ya kisiasa, hali ya uchumi na kukamatwa kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama hicho. Source:Millardayo

WACHEZAJI BORA 4 WAKIKE WA MDA WOTE KATIKA SOKA LA WANAWAKE..(PICHA)

Picha
Mpira wa wanawake ni miongoni mwa michezo inayovutiwa kuangalia ulimwenguni kote sio tu kwa wanawake pia uangaliwa na wanaume, pia kuongezeka kwa Television kuonesha mchezo huo kwa upande wa wanawake ni kutokana na kuvutiwa na kuutangaza zaidi mpira wa miguu kwa wanawake duniani. HAPA CHINI NIMEKUWEKEA  LIST YA WACHEZAZI WANNE  WAKIKE BORA ZAIDI WA MDA WOTE. 1.MARTA (Mshambuliaji,Brazil) 2.MIA HAMM (Mshambuliaji, USA) 3.MICHELLE AKERS (Mshambuliaji/Kiungo Mkabaji, USA) 4.BIRGIT PRINZ (Mshambuliaji/Kiungo mshambuliji, Germany)

Tanzania yaombwa msaada na Uturuki..

Picha
Tanzania imeombwa kuisaidia Uturuki kiwango cha Tani 20 za Korosho kufuatia nchi hiyo kuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo yenye uhitaji zaidi nchini Uturuki, hivyo kupelekea kuomba msaada huo. Ombi hilo limewasilishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka Uturuki ijulikanayo kama ‘Turkish Exportetrs Assembly’ (TIM), Kemal Batuhan Yazici ambapo amesema kuwa, kiwango cha korosho kilichopo nchini kimeshuka wakati mahitaji ya nchi ni Tani 20, hivyo wanaitegemea Tanzania kuondoa uhaba huo nchini mwao. Amesema kuwa Korosho inayohitajika nchini Uturuki ni ile ambayo tayari imechakatwa na kufungashwa vyema kwa viwango vya kimataifa na sio malighafi hivyo ni vyema wafanyabiashara wakaandaa utaratibu wa haraka kuhakikisha Korosho zinasafirishwa kutoka Tanzania kwenda nchini Uturuki. Aidha, Kemal amesema kuwa kwa muda wa miezi sita, kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Uturuki kimeongezeka kwa asilimia 9 kwa bidhaa za Tanzania zinazosafirishwa kutoka nchini Tanzania k...

Mbwana Samatta ameanza msimu wa 2017/18 Ubelgiji kwa kuifungia goli Genk..

Picha
Nahodha wa timu ya taifa ya  Tanzania Taifa Stars   Mbwana Samatta  leo Jumamosi ya July 29 ameingia uwanjani kuichezea timu yake ya  KRC Genk  katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu  Ubelgiji  msimu wa 2017/18 dhidi ya  Waasland Beveren . KRC Genk  leo imecheza game yake ya kwanza katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya  Waasland Beveren  na kulazimishwa sare ya kufungana magoli 3-3, magoli ya  Genk yakifungwa na  Jose Naranjo   dakika ya 70,  Mbwana Samatta  dakika ya 80 na dakika ya 82  Shrivjers  akafunga goli la mwisho. Magoli ya  Waasland  yamefungwa na  Olivier Myny  dakika ya 45,  Zinho Gano  dakika ya 47 na 90, sare hiyo sasa inakuwa ni sare ya pili mfululizo kwa timu hizo toka zilipokutana mara ya mwisho February 7 2017 na kutoma sare tasa,  Genk ...

HEADING ZA MAGAZETI YA LEO JULY 30,2017 KUTOKA KATIKA MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA TANZANIA..

Picha

Waziri Mkuu Azindua Meli mbili zilizonunuliwa na Serikali Mkoani Mbeya..

Picha
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amezindua Meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye Ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya. Amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Nyasa. Amesema kuwa ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo awali suala hilo lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni. Waziri Mkuu amezindua meli hizo zilizojengwa na kampuni ya Kitanzania ya M/S Songoro  Marine Transport mapema hii leo katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya. Aidha, amesema kuwa Meli hizo zitumike katika...

Chelsea yashindwa kutamba mbele ya Inter Milan..

Picha
Chelsea wamemaliza ziara yao ya kujiandaa na msimu ujao kwa kuambulia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Inter Milan katika mchezo uliopigwa leo hii nchini Singapore. Stevan Jovetic alitangulia kuipatia Inter Milan katika dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya Cesar Azpilicueta kumuangusha Jovetic katika eneo  la hatari. Mchezaji anayewindwa kwa karibu na klabu ya Manchester United Ivan Perisic aliifungia bao la pili Inter Milan katika dakika ya 53 kabla ya Geoffrey Kondogbia wa Inter Milan kujifunga dakika ya 74. Bao alilojifunga Geoffrey Kondogba ni moja kati tukio la kushangaza kutokana na mchezaji huyo kupiga mpira kutoka umbali wa mita 45 ulioelekea langoni mwake na kutinga wavuni. Katika mchezo huo kocha Antonio Conte alipanga kikosi cha nguvu huku katika safu ya ushambuliaji akimuanzisha mshambuliaji wake mpya Alvaro Morata aliyecheza na mbeligiji Michy Batshuayi pamoja na mbrazili Willian. \ Source:Dar24 ...