CHAWAUMAVITA kuaadhimisha siku ya CP Duniani.

Na GEOFREY ESTON



CHAMA cha Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA),kitafanya maadhizimisho ya siku ya CP Duniani katika Viwanja vya Mnazi mmoja oktoba 2 mwaka huu Jijini Dar es salaam.

Kikiwa  na lengo la kusaidiana na Taasisi nyingine kwa kupunguza changamoto zinazowakabili watoto wenye Ulemavu na kutafuta njia za kuwasaidia watoto hao, maadhimisho ya siku ya CP Duniani hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni mwendelezo wa mwaka jana "CHANGE MY WORLD IN ONE MINUTE".

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Jonathan Kawamala, ameeleza Dira ya chama chao ni kuchangia upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,akili na Viungo Tanzania ili kuhakikisha watoto wenye ulemevu wa Mtindio wa Ubongo akili na viungo wanasaidiwa kukabiliana na changamoto zilizopo na kuandaa mazingira bora ya makuzi na maisha yao kwa ujumla.

Kawamala alisema katika maadhimisho ya mwaka huu wanatarajia kuwa na mgeni rasmi  ambaye atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB), muda wa saa tatu hadi saa saba mchana.

"Tunawakaribisha wazazi wote wenye watoto wenye ulemavu wa mtindio wa Ubongo,akili na viungo  na siyo wenye matatizo tu bali  watu wote  tunawakaribisha katika maadhimisho haya" Alisema.

Kawamala aliongeza kwamba inadaiwa mtoto mmoja kati ya wanne ambao wana cp hawawezi kuongea na mtoto mmoja kati ya watatu wana cp hawezi kutembea na mtoto  mmoja kati ya wawili ambao wana cp ana taahira ya akili.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..