Mzee aliyechora Nembo ya Taifa amefariki



Taarifa kutoka Hospitali ya Muhimbili zinasema mzee Francis Kanyasu maarufu kama Ngosha, ambaye amehusika kwenye kuchora Nembo ya Taifa Tanzania, amefariki dunia akiwa kwenye matibabu hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa taarifa inaelezwa kuwa May 29, 2017 hali ya mzee huyo ilibadilika ghafla na madaktari walijitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kunusuru maisha yake lakini ilishindikana na akafariki duniani saa 2 usiku.
Mwili wa mzee huyo upo chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo ambapo unasubiri mamlaka husika kutoa maelekezo zaidi.














































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Orodha ya nchi 10 zaidi duniani zenye idadi kubwa ya watu kuliko nchi nyingine (2000-2015) na Nigeria ikiwa ndio nchi ya pekee kutoka bara la Afrika

Wachezaji Ligi Kuu wakatiwa Bima ya Afya...