Tabia 7 Zitakazo Kufanya Uendelee Kuwa Maskini, Hata Kama Una kipato Kikubwa..
Matumaini yangu umeianza siku ya leo ukiwa na afya tele na pia una hamasa kubwa ya kujifunza kama ilivyokawaida. Nami bila choyo yoyote nakukaribisha katika darasa kuweza kujifunza. Leo katika makala yetu ya leo naomba nianze kwa kukuuliza swali, hivi umeshawahi kujiuliza ni kwa nini kuna wakati unaweza ukawa una pesa lakini unashangaa hizo pesa kwa kipindi kifupi tu hauna tena na huelewi hata zimeishaje au zimetumikaje? Tena inawezekana pesa hizo ukawa umezipata za mshahara au za biashara ya aina fulani lakini kitu cha kushangaza kwa muda mfupi hizo pesa huna tena hakuna cha maana ulichonunua. Ni kitu ambacho mara nyingi kinawashangaza wengi na kushindwa kuelewa hizo pesa zimetumikaje hadi kuisha. Naamini pia ni jambo ambalo limewahi kukutokea kwa namna moja au nyingine na kukuacha ukiwa kwenye maswali mengi sana bila kupata majibu. Lakini kama hukujua sababu hiyo isiwe tabu sana kwako. Hali hiyo mara nyingi inasababishwa kwako na kitu kimoja tu ...