Machapisho

Wanariadha wala sabuni wakidhania ni chakula..

Picha
Sabuni Wanariadha waliokuwa wanakimbia mbio ndefu za marathon walijikuta wamekula sabuni baada ya kudhania kwamba zilikuwa chakula kutokana na kukosa kuelewa lugha ya kiingereza. Takriban wanariadha 20,000 katika mbio za Qinyuan marathon kusini mwa mkoa wa Guangdong nchini Uchina walipata zawadi mda mfupi baada ya kumaliza mbo hizo katika utepe kulingana na gazeti la kila siku nchini humo la Peoples daily. Wakidhania kwamba walikuwa wanakula chakula,wanariadha hao badala yake walikuwa sabuni zilokuwa zikinukia harufu nzuri . Walioshuhudia wanasema kuwa sabuni nyingi zilitupwa kandokando ya barabara huku zikiwa zimeumwa. Tatizo ni kwamba sabuni hizo zilikuwa zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na hivyobasi wanariadha hao hawakuelewa lugha hiyo kulingana na gazeti hilo. Hatahivyo walioandaa mbio hizo waliomba msamaha.Pakiti za sabuni hizo zilikuwa kama zile za chakula. Sabuni zilizowekwa katika pakiti na kunuka vizuri kama chakula Pia kulikuwa na wasiwasi kuhusu id...

Ujumbe wa Kibonzo cha leo na Taswira Blog..

Picha

Jumuiya ya kimataifa inaelekea kukosa uvumilivu..

Picha
Viongozi wanaosimamia zoezi la usitishwaji mapigano nchini Sudani Kusini wamevionya vikosi vya pande mbili zinazokinzana nchini humo kuwa jumuiya ya kimataifa inaelekea kukosa uvumilivu kufuatia hatua yao ya kushindwa kutekeleza mkataba wa amani walioutia saini miezi 7 iliyopita. Mkuu wa ujumbe unaosimamia utekelezwaji wa makubaliano ya amani, rais wa zamani wa Botswana, Festus Mogae, amesema timu yake itahakikisha mkataba huo wa amani uliotiswa saini mwezi August mwaka jana unatekelezwa licha ya mapigano kuendelea kushudiwa. Rais Mogae, amezionya pande hizo na kuongeza kuwa kutotekeleza mkataba wa amani walioutia saini ni kuijaribu jumuiya ya kimataifa na kwamba uvumilivu wake unaelekea kufikia mwisho. Source:Focusmedia

Video za Justin Bieber zatazamwa mara bilioni 10..

Picha
Justin Bieber Mwanamuziki Justin Bieber amevunja rekodi ya Vevo kwa video yake kutazamwa mara bilioni 10. Msanii huyo wa Canada ambaye alitoa kibao kipya Purpose in Novemba alipata idadi hiyo katika kipindi cha miaka sita na miezi mitatu au siku 2,316. Kutazamwa kwa video zake mara bilioni 4 kulifanyika baada ya Septemba mwaka jana na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa katika kilele cha chati ya muziki katika Vevo kwa wiki 19 mfululizo. Justin Bieber,Katy Perry na Taylor Swift ni wasanii pekee wenye video mbili tofauti zilizotazamwa zaidi ya mara bilioni moja kila moja. Katy Perry Lakini video yake ya What Do You Mean?Itafikisha kutazamwa mara bilioni moja katika kipindi cha wiki chache zijazo,na kumfanya kuwa msanii wa kwanza kuwa na video tatu zilizotazamwa mara bilioni moja. Mnamo mwezi Januari ,David Bowie alivunja rekodi ya Vevo kwa siku moja. Video zake ziliangaliwa mara milioni 51 baada ya kutangazwa kwamba amefariki akiwa na umri wa miak 69....

Akamatwa kwa kuipeleleza Korea Kusini..

Picha
Kim Dong Chul Raia wa Marekani aliyekamatwa nchini Korea Kaskazini amesema kuwa aliiba siri za kijeshi za Korea kaskazini ili kuisaidia Korea Kusini katika taarifa na waandishi wa habari ilioandaliwa na Pyongyang. Kim Dong Chul mwenye umri wa miaka 62 alikiri kufanya hivyo siku ya ijumaa,akiomba msamaha kwa kupeleleza. Bwana Kim awali aliwaambia waandishi kwamba yeye ni raia wa Marekani aliyezaliwa nchini Korea Kusini na kwamba alikamatwa mwezi Oktoba kwa kufanya upelelezi. Kim Dong Chul Bwana Kim amesema kwamba alikutakana na maafisa wa upelelezi kutoka Korea Kusini mwaka 2011 ili kuifanyia uchunguzi,kulingana na shirika la habari la KCNA kutoka nchini Korea Kaskazini. Alikamatwa wakati alipokuwa akichukua habari za kijasusi za kijeshi na zile za kinyuklia kutoka kwa mtu ambaye hakutajwa. Source:BBC ...

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA IJUMAA KUU LEO JIJINI DAR ES SALAAM (PICHAZ)

Picha
Source:Michuzi blog

App ya Facebook kuondoka simu za Blackberry...

Picha
Maafisa wa Blackberry wameshindwa kushawishi Facebook kubadili msimamo Kampuni ya Facebook imetangaza kwamba app yake haitatumika tena kwenye simu za Blackberry. Uamuzi huo umesikitisha sana kampuni hiyo ya kutengeneza simu Blackberry. Wanaotumia simu hizo za Blackberry watalazimika kutumia visakuzi vya kawaida iwapo wanataka kutumia mtandao huo wa kijamii kwenye simu zao. Bado haijabainika hatua hiyo itatekelezwa lini Mapema mwezi huu, WhatsApp, ambayo humilikiwa na Facebook, ilitangaza pia kwamba simu aina ya Priv za kampuni ya Blackberry. Simu zitakazotupwa na WhatsApp Whatsapp itaacha kutumika katika mfumo wa simu za Blackberry kufikia mwisho wa mwaka 2016. "Tulijaribu sana kushawishi WhatsApp na Facebook wabadilishe msimamo wao, lakini kwa sasa, uamuzi wao haujabadilika,” mtaalamu wa programu za simu wa Blackberry Lou Gazzola, aliandika kwenye blogu. "Tumejibidiisha sana kutafuta njia ya kuwafaa wateja wetu na tunaendelea kutafuta suluhu mbadala...