Seriakali yadaiwa sh6 trilioni..
Jengo la PPF House, jijini Dar es Salaa
Kamati ya Bajeti imesema moja ya eneo ambalo Serikali ina changamoto kubwa ya kutatua madeni yake ni katika mifuko ya jamii yanayofikia zaidi ya Sh6 trilioni.
Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo makamu mwenyekiti Josephat Kandege amesema licha ya Serikali kuonyesha nia njema ya kulipa madeni hayo likiwamo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF bado utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua.
“Mfano kwa mwaka wa fedha 2015/16, Serikali iliahidi kutoa kiasi cha Sh150 bilioni pamoja na kutoa Non Cash Bond ya Sh2.6 trilioni ili kulipa deni la PSPF lakini hadi sasa ni Sh83 bilioni tu zilizotolewa na hakuna Non Cash Bond yoyote iliyotolewa,”amesema Kandege.
Amesema kuwa kamati inaona madeni hayo ni tishio kubwa linaloathiri utekelezaji wa majukumu ya mifuko husika hasa ulipaji wa pensheni ya wastaafu wanaongezeka kila mwaka.
Maoni
Chapisha Maoni