Tanzania ni miongoni mwa nchi za Africa zenye viwanja vichache vya michezo.

Benjamin Mkapa National Stadium in Dar Es Salaam
Kwa mujibu wa tofuti ya 'World Stadiums' Tanzania ni miongoni mwa nchi za Africa zenye viwanja vichache vya michezo ikiwa na jumla ya viwanja 18 tu, tena ni viwanja vya mchezo wa mpira wa miguu ambavyo miongoni mwa viwanja hivyo utumiwa sana katika ligi ya Tanzania maarufu ligi ya Vodacom.

Mara nyingi kiwanja kuitwa kiwanja mpaka kiweze kuwa na vigezo vinavyo staili mpaka kitimie kuwa kiwanja na kutumika katika michezo mbalimbali,kwa Tanzania vigezo hivyo ndio vimeweza kutimia katika viwanja 18 tu kwa nchi nzima na vichache kwa ngazi ya kimataifa.Viwanja hivyo ni kujuhisha Tanzania visiwani 'Zanzibar'.

Kiwanja cha Taifa (National Main Stadium) ambacho kipo katika Jiji la Dar es salaam ndicho kiwanja kikubwa zaidi kuliko viwanja vyote kwa nchi ya Tanzania, ni kiwanja ambacho kinauwezo wa kuchukua watu 60,000; CCM Kilumba  ndicho kiwanja kinachofuatia kwa ukubwa ambacho kipo katika Jiji la Mwanza (Rock City) kinauwezo wa kuchukua watu35,000;kikifuatiwa na kiwanja cha zamani cha Taifa (National Mult-Use Stadium) maarufu kama Shamba la Bibi ambacho nacho kinachukua watu 25,000.

Sheikh Amri Abeid Memorial ni kiwanja kilichopo katika Jiji la Arusha nacho kinauwezo wa kuchukua watu 20,000 tu,Amaan Stadium ni kiwanja kilichopo katika visiwa vya Zanzibar kinachochukua watu 15,000;Sokoine Stadium ni kiwanja kilichopo katika Jiji la Mbeya ambacho kinachukua watu 10,000 na mara nyingi utumiwa na timu za Prison na Mbeya City kwa sasa katika ligi ya Vodacom nchini.

Kwa viwanja vingi vilivyo baki idadi yake ya kuchukuwa watu ni 10,000 na mwisho ni viwanja vinavyo chukua watu 5,000 kikiwemo cha timu ya Azam fc 'Chamazi Stadium' kilichopo katika Jiji la Dar Es Salaam, hivyo ndivyo viwanja vya Jamhuli ya Tanzania vya michezo hasa viwanja vya mpira wa miguu na siyo mchezo mwingine maana Tanzania haina viwanja vya kimataifa vya michezo mingine kama mbio za magari, mpira wa pete, mbio za baiskeli, mpira wa kikapu.

Kama Nchi inapaswa kutizama kwa umakini katika kujenga viwanja vingine vya michezo ili kuweza kuboresha michezo nchini hasa katika michezo mingine zaidi ya mchezo wa mpira wa miguu basi waweze kujaribu kwa michezo mingine kwa kujenga viwanja husika ilikuweza kuboresha michezo mingine tukajulikana kimataifa zaidi.

CCM Kirumba Stadium in Mwanza
Huu ndio muonekano wa nje wa kiwanja cha CCM Kilumba  kilichopo katika Jiji la Mwanza kinacho chukua watu 35,000 ndicho kiwanja cha pili kwa ukubwa wa kuchukuwa watu baada ya Uwanja wa Taifa (National Main Stadium) wa Jijini Dar es salaam.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..