SIRI KUBWA YA DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA VIDEO KALI
Meneja wa staa wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ambaye amekuwa akiachia kazi zenye ubora unaostahili tangu alipo ingia kwenye ramani ya muziki wa bongo fleva ameimbia www.mtembezi.com siri nyingine ya Diamond Platnumz kufanya video kali licha ya kuwa anafanya kazi na ma ‘Director’ wa nje ya Tanzania. Meneja wa Diamond ambaye ni Hamisi Tale A.K.A Babu Tale amesema Diamond ni mtu ambaye anapenda vitu vizuri na hivyo anapofikiria kufanya jambo lake huwa anatenga bajeti mara mbili ya kitu anachotaka kukifanya. “Kwa mfano Diamond unapo mwambia hiki kitu ni laki moja, halafu kizuri zaidi yake ni laki tatu huwa hasiti kutoa ili apate chenye ubora wa juu kwa kuwa muda wote huwa anawa wazia mashabiki zake kuwapa vitu vizuri…” alisema Tale Licha ya Diamond kuwa na tabia ya kutenga bajeti ya juu kwenye kazi zake, Meneja Tale alinogesha kuwa kuna wakati Diamond hapokei video ambayo hajarizika nayo licha menejimenti nzima kuikubali. Babu Tale aliitolea mfano ...