Viongozi Afrika Mashariki Wataka Uchaguzi Burundi Uhairishwe
Viongozi wa Afrika Mashariki, wamesema uchaguzi wa Burundi, unapaswa kuahirishwa kwa angalau wiki sita. Taarifa iliyotolewa kufuatia mkutano wa dharura wa kikanda jana Jumapili, imezitaka pande zote kusitisha ghasia, ikiwa ni kuondoa silaha kutoka kwa vikundi vya vijana na kuwekwa kwa mazingira ya kuwarudisha wakimbizi ambao wamekimbia ghasia za kisiasa. Waziri wa mambo ya nje wa Burundi alimuwakilisha rais Pierre Nkurunziza ambaye hakuhudhuria mkutano huo. Mawaziri kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda na rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma walihudhuria pia mkutano uliofanyika Dar es salaam, nchini Tanzania. Source(VOA)