SAMATTA AISOGEZA TP MAZEMBE KWENYE UBINGWA WA AFRIKA..
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anaekipiga kwenye timu ya TP Mazembe ya Congo DR usiku wa Jumamosi November 1 kuamkia Jumapili aliisaidia klabu yake kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya USM Alger ugenini wakati wa mchezo wa kwanza wa fainali ya klabu bingwa Afrika (Africa Champions League) uliochezwa kwenye kwenye uwanja wa Omar Hamad, Algiers nchini Algeria. Kiungo mshambuliaji wa TP Mazembe na timu ya taifa ya Zambia Rainford Kalaba alianza kuifungia Mazembe goli la kwanza dakika ya 27 kipindi cha kwanza kwa shuti kali akiwa zaidi ya umbali wa mita 25 kutoka golini. Lakini dakika chache baadaye, Kalaba alipata kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga mchezaji wa USM na kupelekea Mazembe kucheza wakiwa pungufu kwa muda wote uliosalia kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili TP Mazembe walipata mkwaju mwingine wa penati baada ya mchezaji wa USM kuushika mpira kwa makusudi akiwa kwenye eneo la hatari na kumzuia Samatta kufunga. Mwamuzi wa mchezo huo Gehad Grisha kutoka Misri alimtoa...