NEYMAR KUIRUDISHA BALLON d’Or BRAZIL?
Kwa mara ya kwanza mshambuliaji mahiri wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar da Silva Santos amefanikiwa kuingia katika tatu bora ya wachezaji wanaowania tunzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon d’Or . Neymar ambaye amekuwa na msimu mzuri katika kikosi chake cha Barcelona na timu ya taifa Brazil ametajwa katika orodha hiyo sambamba na Lionel Messi na mshindi wa tunzo hiyo katika msimu uliopita Christiano Ronaldo. Taarifa katika wavuti ya shirikisho la soka duniani FIFA ,imebainisha kuwa zoezi la kuwapata wanandinga hao limeendeshwa kwa kupigiwa kura na makocha na manahodha wa timu zote za taifa 207 ambao ni wanachama wa FIFA. Kuingia kwa kinda huyu wa kibrazili kunaweka historia ya kipekee katika taifa la Brazili ambalo kwa muda mrefu wachezaji wake hawakuwahi kuingia katika orodha ya tatu bora ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia(mara ya mwisho Ricardo Kaka 2007) Aidha kuingia kwa mara ya kwanza kwa Neymar ni sawa na kutimia kwa...