Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2015

SIRI KUBWA YA DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA VIDEO KALI

Picha
Meneja wa staa wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ambaye amekuwa akiachia kazi zenye ubora unaostahili tangu alipo ingia kwenye ramani ya  muziki wa bongo fleva ameimbia  www.mtembezi.com  siri nyingine ya Diamond Platnumz kufanya video kali licha ya kuwa anafanya kazi na ma ‘Director’ wa nje ya Tanzania. Meneja wa Diamond ambaye ni Hamisi Tale A.K.A Babu Tale amesema Diamond ni mtu ambaye anapenda vitu vizuri na hivyo anapofikiria kufanya jambo lake huwa anatenga bajeti mara mbili ya kitu anachotaka kukifanya. “Kwa mfano Diamond unapo mwambia hiki kitu ni laki moja, halafu kizuri zaidi yake ni laki tatu huwa hasiti kutoa ili apate chenye ubora wa juu kwa kuwa muda wote huwa anawa wazia mashabiki zake kuwapa vitu vizuri…” alisema Tale Licha ya Diamond kuwa na tabia ya kutenga bajeti ya juu kwenye kazi zake, Meneja Tale alinogesha kuwa kuna wakati Diamond hapokei video ambayo hajarizika nayo licha menejimenti nzima kuikubali. Babu Tale aliitolea mfano ...

PAM D AKISIFIA KICHUPA CHA POPOLIPOPO..

Picha
Msanii mahiri  nchini Tanzania ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na Swaga za kipekee anazo zitumia kwenye nyimbo zake Pam D, yupo mbioni kuachia kichupa chake cha Popolipopo alichomshirikisha binamu yake ambaye pia ni msanii mahiri na mtayarishaji wa mziki mzuri Mesen Selekta. Akizungumza na www.mtembezi.com Pam D amesema kuwa video ya Popolipopo ni moja ya video kali anazo ziheshimu katika maisha yake ambapo anaimani itamfikisha mbali, kutokana usimamizi mzuri wa Travellah wa Kwetu Studios. hivyo amewataka wadau wa mziki waipokee video hiyo na kumuunga mkono. SOURCE:Mtembezi.com

Zaidi ya shilingi Bilioni 500 zinahitajika kutatua changamoto za upatikanaji wa dawa Nchini..

Picha
Tanzania inahitaji zaidi ya shilingi bilioni mia tano kwa ajili ya kutatua changamoto za upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya, zahanati na Hospitali mbalimbali za serikali hapa nchini. Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya dawa nchini ( MSD ) Laurean Rugambwa Bwana. Kunu amesema upatikanaji wa fedha hizo utaiwezesha Bohari hiyo kusambaza dawa nchini ili kuwawezesha wananchi kupata dawa kwa bei nafuu, ambapo katika mkoa wa Mwanza MSD imekamilisha maandalizi ya kufungua duka la dawa katika Hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure,ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dk.John Pombe Magufuli.    Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Dk.Faisal Issa amesema kuwa ongezeko la mapato ya serikali yatasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo.  Awali meneja wa MSD kanda ya ziwa Byekwaso Tabura pamoja na mganga mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure Dk.Onesmo Rwakendera wamesema kufunguliwa kwa duka hilo la dawa katika...

Mlipuko wa kipindupindu Malawi..

Picha
Mlipuko wa ugonjwa huo umechangiwa pakubwa na hali duni ya usafi wa mazingira katika eneo la ziwa Chilwa. Nchi ya Malawi imekumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, miezi miwili tu baada ya msimu wa mvua kuanza. Mamlaka za Afya nchini humo zinasema ugonjwa huo umeathiri wakaazi wengi katika wilaya tatu zinazozingira ziwa Malawi. Milipuko ya kwanza ya kipindupindu iliripotiwa katikati ya mwezi  katika Machinga na Zomba mashariki mwa wilaya za Machinga na Zomba ambako mtu mmoja alifariki na wengine 26 kulazwa mahospitalini. Maafisa wa Wizara ya Afya nchini Malawi waliiambia Sauti Ya Amerika Jumatano kwamba ugonjwa huo, ambao husambazwa kupitia maji, unaenea kwa kasi, huku kukiwa na visa 95 vilivyoripotiwa. Wanasema mlipuko wa ugonjwa huo umechangiwa pakubwa na hali duni ya usafi wa mazingira katika eneo la ziwa Chilwa. Andrian Chimbuke ni msemaji wa wizara ya afya. Anasema: “Katika ziwa Chilwa, watu wana mazoea ya kujenga manyumba karibu sana na maji…h...

Watumishi wa Umma Watakiwa Kutumia Mfumo Rasmin wa Barua PEPE..

Picha
Waziri    Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam. Waziri   Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es salaam. Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri    Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) kuhusu utendaji wa Wakala hiyo leo wakati wa    ziara ya kikazi ya Mhe. Angella Kairuki katika Ofisi za Wakala hiyo leo jijini Dar es salaam.   Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri    Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma...

TCRA YASHUSHA RUNGU KWA TIGO,AIRTEL,ZANTEL,SMART NA HOLATEL KWA KISA HIKI...

Picha
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI HATUA ZA KISHERIA NA KIUDHIBITI KWA MAKAMPUNI YA SIMU YALIYOSHINDWA KULINDA WATEJA WAKE KITEKNOLOJIA NA KISHERIA KUHAKIKISHA USALAMA WA MAWASILIANO YAO 1. Katika shughuili zake za udhibiti wa huduma za mawasiliano nchini, Mamlaka ya Mawasilaino Tanzania imepokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya kuwepo mazingira yasiyo salama katika huduma za mawasiliano na hivyo kusababisha kufanyika kwa vitendo vya utapeli unaofanywa kwa kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai, hivyo kusababisha watu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.  Kwa mfano kupokea ujumbe kutoka namba unayoifahamu ukikuagiza utume fedha au ujumbe wa kashfa au matusi wakati hautoki kwa mhusika mwenye namba. Mamlaka imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja na malalamiko mengine hupelekwa Polisi. Kwa miezi miwili tu, matukio 42 yameripotiwa Polisi pamoja na TCRA ambayo tukio moja tu linakuwa na ulaghai wa takribani milioni 25 peke yake. 2...

MB DOG: NATARAJIA KUFANYA COLLABO NA LIL WAYNE.

Picha
Msanii Mb Dog anatarajia kufanya kazi na msanii mkubwa wa hip hop kutoka Marekani Lil Wayne, mara baada ya makubaliano kukamilika. Mb Dog ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa meneja wake yupo safarini, na moja ya jambo atalofanya ni kuongea na Lil Wayne ili kuweza kufanya nae kazi.  “QS Mhonda yuko safarini, anafanya maongezi na Lil Wayne, tunasubiri kupata clip kidogo tuwaletee, unajua mwenye mawazo madogo wanawaza hivyo, kwa sababu Lil Wayne mtu tu kati ya watu” , alisema Mb Dog.  Pamoja na hayo Mb Dog amesema yeye anapofanya colabo na wasanii wanaofanya vizuri sasa hivi sio kama anatafuta njia ya kurudi, bali anachanganya ladha na kutanua soko la kimataifa.  “Kushirikisha sio sababu ya kutoka, ni kuchanganya ladha kwa sababu nilishatokaga, tena mwenyewe, kwa sasa hivi nategemea kushirikisha mtu ili kutoka kimataifa” , alisema Mb Dog.  Pia Mb Dog amesema kazi ambayo...

Waziri mkuu aagiza watumishi kwenye halmashauri kuzingatia weledi na uadiliu kazini.

Picha
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa amewaagiza watendaji wa halmashauri nchini kutenda kazi kwa uadilifu na kuzingatia maelekezo ya viongozi wa juu ili kuleta tija na kwamba serikali haitamvumilia mtumishi wa umma mzembe, mvivu na asiye muadilifu. Mh Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma, viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Kigoma, ambapo amesema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kikamilifu na kwa wakati.  Aidha ameagiza kila halmashauri nchini  kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwakani wanaanza masomo yao kwa asilimia mia moja ambapo kwa mkoa wa Kigoma amesema serikali itaimarisha ulinzi katika ziwa Tanganyika ili kuondoa uporaji wa zana za uvuvi na ametoa siku mbili kwa mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma ujiji Boniphace Nyambele, Mhandisi na mweka hazina kutoa taarifa kwa katibu tawala mkoa juu ya uuzwaji...

Profesa Muhongo anusa rushwa Rea mkoani Kagera..

Picha
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo       Bukoba.  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amenusa rushwa katika Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) ya njia za uunganishaji umeme zinazochepushwa, huku taasisi za dini na wananchi wakitozwa fedha kinyume cha utaratibu ili waunganishiwe nishati hiyo. Kutokana na kubaini hilo, Profesa Muhongo ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza suala hilo, akisema amepokea malalamiko mengi ya wananchi na kutoa mfano wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera ambako kanisa moja lilitakiwa kutoa rushwa. Alisema wananchi wanatozwa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na maelekezo na kuagiza waanze kupewa elimu ili wafahamu taratibu za kufuata kabla ya kuunganishiwa umeme. Profesa Muhongo aliutaja Mkoa wa Kagera kuwa unaongoza kwa malalamiko. Akiwa mjini Bukoba baada ya ziara yake ya siku mbili, alizionya kampuni zilizopewa kandarasi ya kusambaza umeme na kulalamikiwa n...