Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2016

MAREKANI YAFANIKIWA KUIFUNGUA i Phone YA MLIPUAJI..

Picha
Wizara ya Sheria ya Marekani imesema imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone mali ya mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple. Wakili wa Marekani Eileen Decker alisema kuna mtu aliisaidia idara hiyo kuifungua Simu hiyo ya iPhone bila kuathiri data zilizohifadhiwa. Kampuni ya Apple ilikataa kusaidia uchunguzi , kwa kusema ni kuweka ‘ historia mbaya. Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye, pamoja na mke wake, waliuua watu kumi na wanne kusini mwa California Desemba mwaka jana. Source:Mtembezi.com

TTCL KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 400...

Picha
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ipo kwenye maandalizi ya kupunguza wafanyakazi wasiohitajika kwa sasa kutokana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia. TTCL inayotoa huduma za simu na pia kutoa mitandao kwa kampuni zilizo na leseni ya huduma hizo, itapunguza wafanyakazi 400 ili kuongeza ufanisi na hivyo kumudu ushindani katika sekta ya mawasiliano dhidi ya kampuni binafsi.  Mapema mwaka jana, Serikali iliamua kununua asilimia 35 ya hisa za TTCL zinazoshikiliwa na kampuni kubwa ya huduma za simu nchini India, Bharti Airtel na baadaye mwezi Mei, 2015 aliyekuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano, January Makamba aliliambia Bunge kuwa Serikali iko katika maandalizi ya mwisho ya kumiliki hisa zote za kampuni hiyo kubwa kwa huduma za simu za mezani nchini. Chanzo cha habari kutoka ndani ya kampuni hiyo kinaeleza kuwa kati ya wafanyakazi 1,500 wa TTCL, zaidi ya 400 watapoteza ajira katika mpango huo wa kudhibiti gharama za uendeshaji. “TTCL itaomba fedha ili kuwalipa...

Tanzania yalalama, Zanzibar yasema sawa, ni kuhusu MCC..

Picha
Balozi Seif Ali Iddi, makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Tanzania imezungumzia sakata la usitishwaji wa fedha za msaada awamu ya pili kutoka mfuko wa changamoto za millenia (MCC) kiasi cha dola Milioni 472 kutokana na Tanzania kutotimiza sifa za kupatiwa fedha hizo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, amesema msaada huo umesitishwa na bodi ya MCC  kutokana na Tanzania kupoteza sifa. Hii ni kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana kwa upande wa Zanzibar pamoja na utekelezwaji wa sheria ya makosa ya kimtandao. Tanzania imesema haiwezi kulalamikia ushitishwaji wa msaada huo kwavile uamuzi wa kuzitoa na kusitisha ni wa bodi yenyewe. Balozi Mahiga amesema kutopatikana kwa fedha hizo kutaathiri Tanzania kufikia malengo endelevu ya milenia katika miradi iliyokuwa inahusika na msaada huo hususani miradi ya nis...

Peter na Paul Okoye wanounda kundi la P-square wameungana tena na kufanya show kali huko nchini Uholanzi.(PICAHZ)

Picha
P-square walitumbuiza katika tamasha la Palmundo World Festival , huko katika mji wa Rotterdam Nchini Uholanzi.

Brussels: Aliyeghushi vyeti vya usafiri anaswa..

Picha
Brussels: Aliyeghushi vyeti vya usafiri anaswa Polisi wa Italia wamemkamata mwanamume mmoja kutoka Algeria, ambaye anashukiwa kughushi vitambulisho vya bandia, ambavyo vilitumiwa na washambuliaji wa mjini Paris na Brussels. Djamal Eddine Ouali, mwenye umri wa miaka 40, alikamatwa kufuatana na amri ya Umoja wa Ulaya, karibu na Salerno, kusini mwa Utaliana. Ripoti zinasema kuwa jina lake lilipatikana kwenye nyaraka, zilizopatikana wakati nyumba moja ya mjini Brussels, ilipovamiwa mwezi wa Oktoba mwaka jana. Djamal Eddine Ouali, mwenye umri wa miaka 40, alikamatwa kufuatana na amri ya Umoja wa Ulaya Jina la bwana huyo pamoja na picha za wapiganaji, ambao baadaye walifanya mashambulio mjini Paris na Brussels.

Kansa yachukua maisha ya mwanasoka mwingine – Abel Dhaira Afariki Dunia..

Picha
Dunia ya soka imepata msiba mwingine siku kadhaa baada ya kifo cha Johan Cruyff, wana afrika mashariki tuna Msiba mwingine. – golikipa wa zamani wa Simba, Abel Dhaira hatunae tena.   Golikipa huyo aliyekuwa na miaka 28 aligundulika kuwa na kansa ya tumbo mwanzoni mwa mwaka huu.  Kifo chake kimekuja wakati ambao mkataba wake wa bima ya afya katika klabu ya  IBV Vestmanaeyjar ya Iceland – ulikuwa unamalizika.  Dhaira alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Walukuba  ya jijini Jinja. Baada ya hapo alihamia Express, kisha akaenda URA kabla ya kuja kujiunga na Simba Sports Club ya Tanzania.  Aliitumikia klabu ya IBV Vestmanaeyjar football club inayoshiriki ligi ya Iceland premier league mpaka kifo chake.   Source:Shaffihdauda.com

TIMU YA CHAD IMEJITOA MICHUANO YA AFCON..

Picha
Timu ya taifa ya chad imejitoa katika mashindano ya kugombania nafasi ya kucheza fainali ya michuano ya mataifa ya Africa itakayo pigwa Gabon   BARUA YA CHAD Chad imeshindwa kufika Jjini Dar es salaam kwa kile walicho eleza kuwa  nchi yao imeyumba kiuchumi kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani kuikumba nchi hiyo Hivyo mchezo wake na Taifa Stars uliopangwa kufanyika kesho hautokuwepo na kwa mujibu wa sheria  ya Tanzania, huenda Taifa Stars itapewa mogoli 2 na alama tatu hivyo kufikisha alama 7 kujitoa kwa chadi kuna liweka kundi G liwe gumu sana “Timu yetu haiwezi kusafiru hadi Dar es salaam kwa mechi ya tarehe 28, nchi yetu imeathirika na mgogoro wa uchumi duniani,hivyo ushiriki wetu kwenye mashindano mbali mbali umepata pigo kubwa kutokana na ukosefu wa fedha, tunaomba radhi kwa usumbufu”   Taarifa  ya chama cha soka nchini Chad imeeleza. Taarifa hii imeripotiwa na mtandao wa Supersports.com mapema leo Source:Mtembezi.com ...

MAGAZETI YA LEO MARCH 27.2016 VICHWA MBALIMBALI VYA HABARI VILIVYOANDIKWA KUTOKA KATIKA MAGAZETI TOFAUTI YA HAPA NCHINI.

Picha
Leo March 27/2016 nimekuwekea magazeti mbalimbali ya hapa nchini amabayo Taswira imeweza kuyapata na kukusogezea ww msomaji wa Blog hii ilikujua kilichojiri katika magazeti ya leo ya hapa nchini Tanzania.

HABARI MBALIMBALI KUTOKA TWITTER ZILIZOANDIKWA SIKU NZIMA YA LEO KUTOKA KATIKA MEDIA TOFAUTI..

Picha
Ni habari zilizoandikwa na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchi na hata nje ya nchi siku nzima ya leo ambapo Taswira blog haijaweza kuzipata kwa wakati.

VANESSA MDEE AFUNGUKA JUU YA UVAAJI WAKE WA NUSU UTUPU, ASEMA ANATANGAZA BRAND...!!!

Picha
Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye anafanya poa katika anga za kimataifa na sasa anatamba na kibao chake cha  "Niroge"  Vanesa mdee , amefunguka sababu ya yeye kupenda kuvaa nguo za nusu utupu. Akiwa kwenye kipindi cha  Friday Night Live  kinachorushwa na  East Africa Radio  na  EATV , Vanessa Mdee amesema anapenda kuvaa mavazi hayo ambayo hayakubaliki kwa jamii, kwa sababu anatangaza brand yake, na hatimaye impe dili la matangazo kwa wabunifu wa mavazi. “Ukweli ni huu, wasanii for a long time in the past, wasanii wa kitanzania hawajajua na kutambua brand yao, mi brand yangu mi nataka ndani ya miaka miwili napigiwa simu na Balmain, na Lui V, nataka dersigners wakubwa wa dunia wanitumie kutangaza bidhaa yao kwa sababu wanaamini nina brand yangu kubwa na zinaendana, so nna malengo , na if im gonna offend any body im sory” , alisema Vanessa Mdee. Vanessa Mdee ambaye kwa sasa ameachia video yake mpya ya Niroge , amesema ana mipango ya...

Salah ainusuru Misri dhidi ya Nigeria..

Picha
Mohammed Salah alifunga katika dakika za majeruhi na kuinusuru Misri kupata pointi moja ugenini dhidi ya Nigeria katika mechi ya kufuzu kwa kombe la Afrika mwaka 2017. Matokeo hayo sasa yanaiweka Misri katika kilele cha kundi G ikiwa na pointi mbili juu ya Nigeria. The Super Eagles walichukua uongozi kupitia mshambuliaji wa timu ya Warri Wolves Etebo Oghenekaro lakini kiungo wa kati wa Roma Salah akasawazisha katika dakika ya 91. Timu mbili za juu katika kila kundi zina fursa ya kufuzu katika raundi ya pili katika harakati za kuelekea Gabon 2017. Source:BBC

KUANGALIA MECHI YA TAIFA STARS NA CHAD BUKU TANO TU..

Picha
Source:Michuzi blog

Adele aomba msamaha baada ya shabiki kujeruhiwa..

Picha
Adele Mwanamuziki wa muziki wa Pop Adele ameomba msamaha baada ya shabiki mmoja kujeruhiwa alipoangukiwa na nyororo katika tamasha la Glasgow. Nyota huyo alikuwa anaendelea na onyesho lake katika ukumbi wa SSE Hydro siku ya ijumaa usiku wakati nyororo hiyo ilipomuangukia mwanamke huyo aliyekuwa amekaa katika eneo la mashabiki. Alichukuliwa na kupelekwa hospitali kama tahadhari kulingana na msemaji wa ukumbi huo. Adele baadaye alituma ujumbe katika mtandao wake wa Tweeter akisema: Pole kwa kusikia kwamba kuna mtu alijeruhiwa katika tamasha yangu usiku. Uchunguzi unaendelea ili kuhakikisha kisa kama hicho hakitokei tena. Source:BBC

Zubeir Ali Maulid spika Mpya Baraza la Wawakilishi Zanzibar..

Picha
Hatimaye wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chama Cha Mapinduzi Zanzibar leo wamefanya Uchaguzi wa kumpata mjumbe atakaye peperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Spika wa Baraza hilo, kwa kipindi cha mwaka 2015 – 2020. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC waIdara ya Itikadi na Uenezi  Mhe. Waride Bakari Jabu, amesema uchaguzi huo ulioendeshwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, ulifanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Unguja. Mwenyekiti wa Uchaguzi huo, uliojumuisha wajumbe 72, alimtangaza Zubeir Ali Maulid (Pichani) kuwa mshindi baada ya kupata kura 55 na kuwashinda wapinzani wake wawili aliyemaliza muda wake Pandu Ameir Kificho aliyepata kura 11 na Jaji Janeth Nora Sekihola aliyepata 4, na kura mbili (2) ziliharibika. Jumla ya wanachama wa tisa (9) walijitokeza kuomba ridhaa ya CCM ili wagombee nafasi hiyo ya Spika . Katika kikao cha Kamati Maalum kilichofanyika Machi 24...