Twiga Stars walazwa na Zimbabwe..

Nasra Mohamed
Kocha wa Twiga Stars Nasra Mohamed akizungumza baada ya mechi.
Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania imelazwa na Zimbabwe kwenye mechi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016.
Twiga Stars wamechapwa 2-1 na Zimbabwe katika mechi iliyochezewa uwanja wa Azam complex jijini Dar es Salaam.
Magoli ya Zimbabwe yamefungwa na mchezaji Elina Jeke mabao yote mawili nalo bao la Twiga Stars likatiwa kimiani na Mwanahamisi Omar.
Takaedza Mugadza
Kocha wa Zimbabwe Takaedza Mugadza.


Mechi ya marudiano itachezwa hivi karibuni mjini Harare nchini Zimbabwe.






Source:BBC





































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Wachezaji Ligi Kuu wakatiwa Bima ya Afya...

Orodha ya nchi 10 zaidi duniani zenye idadi kubwa ya watu kuliko nchi nyingine (2000-2015) na Nigeria ikiwa ndio nchi ya pekee kutoka bara la Afrika