Ziwa Victoria ambalo limesababisha vifo vya watoto wawili huko mkoani Kagera Sikukuu ya Eid el-fitri imeacha majonzi makubwa mkoani Kagera, baada ya familia ya askari wa Kikosi cha Usalama barabarani, Hamis Kachwamba kupoteza watoto mapacha waliofariki dunia baada ya kuzama Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Mapacha hao Hassan na Hussein, waliokuwa na umri wa miaka 12, walikumbwa na mkasa huo saa 11: 25 jana jioni, walipokuwa wakiogelea katika ufukwe wa Ziwa Victoria ikiwa ni sehemu ya kusheherekea za sikukuu ya Eid. Akizungumza na mwandishi wa Azam TV, Junior Mwemezi wa mkoani Kagera, Kamanda wa Jeshi la Polisi, Augustine Olomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo ameliita kuwa ni la kusikitisha. “Kuna tukio moja la watoto wawili wa familia moja walifariki jana baada ya kuzama ndani ya Ziwa Victoria, wakawa wamekufa maji.” alisema Kamanda Olomi Baba mzazi wa watoto hao Hamis Kachwamba, ambaye amezungumza kwa majonzi, amesema alikuwa njiani wakati tukio ...