Canada kutoa chanjo ya majaribio kwa ugonjwa wa Ebola.



Serikali nchini Canada inasema kuwa itatoa hadi dozi 1,000 za chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola kwa shirika la afya ulimwenguni WHO.

Hii ni kwa lengo la kusadia kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika ambao hadi sasa umewaua zaidi ya watu 1,000.
Hatua hii ni baada ya shirika la afya duniani kusema ni sawa kimaadili kutumia dawa ambayo bado inafanayiwa majaribio kutibu wagonjwa katika hali ya dharura.

Waziri wa afya nchini canada Rona Ambrose amesema kuwa nchi hiyo imetengeneza karibu dozi 500 za dawa hiyo lakini haijafanyiwa majaribio kwa binadamu.
Wataalamu wanaonya kuwa huenda ikachukua hadi miezi sita kuunda kiwango cha dawa ambacho kinaweza kutumiwa.

Kamapuni moja wa kimarekani ambayo ilikuwa imetengeneza dawa za majaribio inasema kuwa kwa sasa kiwango cha dawa ilicho nacho ni kidogo.(Chanzo BBC Swahili).










Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..