Europe ndilo bara lenye viwanja vingi kuliko mabara mengine ulimwenguni.


Kwa mujibu wa tovuti ya 'worldstadiums.com' inaonesha bara la Europe ndilo bara la kwanza kuliko mabara mengine lenye viwanja vingi vya michezo ukijumhisha vile vya mpira wa miguu, mbio za magari, baiskeli,basketball,baseball,volleyball na vingine vingi ambavyo sijaweza kuviorozesha ambavyo ujumhisho wake akuna bara lingine lenye idadi hiyo ya viwanja siyo tu kwa viwanja vya mpira bali kwa viwanja kwa michezo yote ambavyo vipo katika nchi za bara hilo.

Welcome to World Stadiums
Europe linaongoza kwa kuwa na viwanja 4,348 ikifuatiwa na bara la North America likiwa na idadi ya viwanja 2,912, Bara la Asia lina idadi ya viwanja 1,621 likiwa ni bara la tatu kwa wingi wa viwanja vya michezo,na bara la mwisho ama la nne katika mabara yenye idadi kubwa ya viwanja vya michezo ambalo ni Bara la South America lenye viwanja 1,439.

Tukiangazia mabara  yenye idadi ndogo ya viwanja vya michezo ni pamoja na Africa likiwa na idadi ya viwanja 784,likifuatia bara la Middle East likiwa na idadi ya viwanja 695,bara la Central America lina idadi ya viwanja 322 na bara la mwisho kabisa ambalo ndio bara lenye idadi ndogo kabisa ya viwanja vya micheo ni bara la Oceania likiwa na jumla ya viwanja 289.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..