Liberia kutumia 'Zmapp' kutibu Ebola


WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia

Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.

Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.
Kuidhinisha utumizi wa dawa ilio katika majaribio ni swala gumu.
Dawa hiyo ambayo haijajaribiwa imetumiwa na raia wawili wa kutoa msaada kutoka marekani ambao afya yao imeimarika,lakini kasisi huyo wa Uhispania ambaye pia aliitumia dawa hiyo ameaga dunia.
Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio liitwalo Zmapp baada ya kuiomba serikali ya Marekani.


Shirika la WHO lilisema kuwa lilikuwa limeombwa kupendekeza hatua hiyo kwa sababu ya kusambaa kwake na idadi kubwa ya vifo.(Kutoka BBC Swahili).

Maoni

  1. Kwa hali hii ya ugonjwa wa Ebola inatupasa nasi tuwemakini kwa janga hili ambalo wenzetu wa nchi za magharibi hasa liberia linawatesa sana ambapo takribani watu 1000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.Ni muhimu kuzijua dariri hizo hili kuweza kuzuia kuto enea kwa kasi nchini kwa wale wachache waliokutwa kutazamwa na kuwekwa sehemu moja na kutibiwa.Ebola inatisha wanatanzania tuwe makini na dariri zake.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..