Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2014

Taswira ya barabara katika maeneo ya Tanesco ubungo jijini Dar es salaam.

Picha
Ni muonekano wa barabara (Morogoro Road)itakayo tumika na mabasi yaendayo kwa kasi jijini humo ikiwa imeanza kukamilika kwa kiasi chake na taswira kwa ujumla ya anga safi lilotanda jijini Dar es salaam.(Picha na Akajanja)

Kutana na uvumbuzi mpya kongo

Picha
Kwa kurahisisha usafiri katika mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo,Kinshasa,mwanasayansi Therese Kirongozi amevumbua roboti za kuongozea magari barabarani kupitia kampuni yake ya Women Technology. Mhandisi Therese Kirongozi akisubiri wataalii wanaotembelea mahala anapotengeneza maroboti ya kurahisisha usafiri.Mwanamke wa kwanza kutengeneza roboti nchini DRC. (Chapisho kutoka DW/Saleh Mwanamilongo).

Ndege ya Aljeria imetoweka na watu 116

Picha
Shirika la ndege la Algeria , Air Algerie, limesema kuwa limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zake ilipokuwa ikitoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou. Ndege hiyo ilikuwa inaelekea mji mkuu wa Algiers, ilikuwa na watu mia na kumi pamoja na wahudumu wa ndege hiyo wakiwa sita,nambari ya ndege hiyo ni AH 5017 inayomilikiwa na shilika la ndege la kihispania la Swiftair. Ndege nambari AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP ni shirika la habari  huko Mali limeripoti.Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti. Mwezi Februari ndege ya kijeshi ya Aljeria ilianguka na kuuwa watu 77 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Miili ya watu waliopata ajari ya ndege imewasili uholanzi

Picha
Ndege mbili za kijeshi zilizobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa ukraine, imewasili uholanzi.(Story na Picha kutoka BBC Swahili).

James Rodriguez ni mchezaji wa tano aliye nunuliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha Ulaya

Picha
James Rodriguez kutoka nchi ya colombia pia alichezea klabu ya Monacco ya kule ufaransa amekuwa mchezaji wa tano kati ya wale walionunuliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha huko ulaya, Rodriguez aling'ara katika mashindano ya kombe la dunia ya mwaka huu (2014) yaliyofanyika huko Brazil na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo, kaweza kununuliwa na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

KABLA YA KIFO CHA BALLALI

Picha
Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania BOT), Marehemu Daudi Ballali aliacha wasia unaotaka maiti yake isionyeshwe hadharani atakapofariki dunia na wala maiti yake isiletwe Tanzania kwa ajili ya maziko. ...