Ndege ya Aljeria imetoweka na watu 116
Shirika la ndege la Algeria , Air Algerie, limesema kuwa limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zake ilipokuwa ikitoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou.
Ndege hiyo ilikuwa inaelekea mji mkuu wa Algiers, ilikuwa na watu mia na kumi pamoja na wahudumu wa ndege hiyo wakiwa sita,nambari ya ndege hiyo ni AH 5017 inayomilikiwa na shilika la ndege la kihispania la Swiftair.
Ndege nambari AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP ni shirika la habari huko Mali limeripoti.Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.
Mwezi Februari ndege ya kijeshi ya Aljeria ilianguka na kuuwa watu 77 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Maoni
Chapisha Maoni