Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2017

Tazama nyimbo mpya ya Mr. Blue Feat JR - Siwezi

Picha

Cassper Nyovest - Destiny [Feat. Goapele] (Official Music Video)

Picha

CHADEMA YAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA KUFUFUA UCHUMI...

Picha
Chama cha Chadema kimevunja ukimya kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi nchini, na kudai kuwa hali ni mbaya huku ikiitaka serikali kuandaa mpango mkakati wa haraka wa kufufua uchumi.  Wakati akisoma tamko la Kamati Kuu ya Chadema leo Julai, 31, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amedai kuwa, tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani uchumi wa taifa umeporomoka kutokana na usimamizi mbovu na maamuzi ya papara katika masuala ya biashara, uwekezaji, uandaaji na utekelezaji wa bajeti. Mbowe ametaja baadhi ya vigezo vinavyoashiria hali ya uchumi kuwa mbaya ikiwemo kudorola kwa sekta ya kilimo na kupelekea bei ya vyakula hasa vya nafaka kupanda, hali ya ukata katika mzunguko wa fedha, kupungua kwa mikopo ya benki za biashara katika sekta muhimu za kiuchumi, na kuongezeka kwa deni la taifa. “Kwa ujumla mwendo wa uchumi wetu ni mbaya mauzo ya nje yameporomoka, manunuzi kutoka nje yameporomoka, mikopo sekta binafsi imeporomoka, deni la taifa linapaa kuliko kipindi ch...

Baada ya kutoweka, Meneja wa ICT ya Tume ya Uchaguzi Kenya akutwa amefariki

Picha
Baada ya kuwepo kwa taarifa za kutoweka ghafla kwa Meneja wa kitengo cha  ICT  ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka Kenya  IEBC,  Chris Musando,  leo July 31, 2017 imeripotiwa amekutwa akiwa amefariki. Imeelezwa kuwa mwili wa  Chris Musando   aliyekuwa Meneja wa masuala ya Teknolojia wa  IEBC,  umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi huku mawasiliano yake ya mwisho yakiwa kwa njia ya SMS na mmoja wa wafanyakazi mwenzake siku ya Jumamosi majira ya saa tisa usiku. Tukio hili linatokea ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Kenya ambao utafanyika tarehe 8 August. Polisi wanasema kuwa miili ya Afisa huyo pamoja na mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo vitongoji vya mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti. Source:Millardayo

HEADING ZA MAGAZETI YA LEO JULY 31,2017 KUTOKA KATIKA MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI..

Picha

Manny Pacquiao ataka kujiunga na vikosi vinavyopigana na magaidi wa ISIS...

Picha
Bondia Manny Pacquiao ambaye pia ni Seneta nchini Ufilipino amevitembelea vikosi vinavyopambana na magaidi wa kundi la ISIS waliolivamia jiji la Marawi nchini humo kwa wiki kumi hadi sasa. Pacquiao alitembelea kikosi kilichoko katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo majira ya saa tatu asubuhi (kwa saa za Ufilipino) akiwa amevalia sare za kikosi maalum cha jeshi la nchi hiyo ambacho kiliwahi kumtunuku ujumbe wa heshima wa kikosi hicho (honorary member). Kwa mujibu wa Rappler, Pacquiao aliwatia moyo wanajeshi wanaopambana katika eneo hilo huku akieleza kuwa ana nia ya kujiunga na vikosi hivyo kusaidia mapambano. “Nataka kujiunga nanyi katika mapambano, mtapenda iwe hivyo. Msirudi nyuma, kwasababu ndivyo ilivyo hata kwenye masumbwi, tuko katika raundi ya 3 lakini ni kama vita imeshakwisha,” Pacquiao anakaririwa na Rappler. “Nyie ndio mashujaa wa kweli, mimi ni bondia tu. Ninyi mmejitolea maisha yenu kwa nchi yetu. Ninaamini nitarudi tena kuwatembelea baada ya kumaliza mapambano....

Simon Msuva ameanza kwa kufunga Morocco game ya kwanza..

Picha
Winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya  Tanzania Taifa Stars   Simon Msuva  aliyekuwa anaichezea  Yanga , Jumapili ya July 30 ikiwa ni siku nne zimepita toka asaini mkataba na timu ya  Difaa El Jadid  ya Morocco, ambapo ni mafanikio kutoka kucheza  Tanzania  nchi iliyopo nafasi ya 114 katika viwango vya  FIF A anakwenda kucheza nchi iliyopo nafasi ya 60. July 30 amepata nafasi ya kuichezea timu yake ya  Jadid  mchezo wa kwanza wa kirafiki na kufunga goli wakipoteza kwa magoli 2-1, kocha wa  Jadid  aliamua kuchezesha vikosi viwili katika mchezo huo ambapo kila kikosi kilicheza kwa dakika 45. Dakika 45 za kwanza kocha wa  El Jadid  alichezesha wachezaji aliyopandisha kutoka team B na wachezaji wanaofanya majaribio ambapo kikosi hicho kilifungwa magoli mawili na ndio dakika 45 za pili  Simon Msuva  na wachezaji wengine wakaingia na  Msuva akafunga goli la kufutia machozi. Source...

Majaliwa awaasa watumishi wanaofanyakazi viwandani..

Picha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu. Majaliwa amesema hayo leo Julai 30, 2017 wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe, amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu. Amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu. “Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.” Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa  katika maeneo yao. Kabla, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi Harold Te...

Makamu wa Rais Kenya azungumzia tukio la uvamizi nyumbani kwake

Picha
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto amezungumzia tukio la watu wenye silaha kuvamia nyumbani kwake jana majira ya mchana na kupambana na vikosi vya usalama. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, watu hao wenye silaha wanadaiwa kuvamia nyumbani kwa Ruto eneo la Sugoi  majira ya saa saba mchana na kwamba baada ya kumzidi nguvu mlinzi aliyekuwa getini waliingia ndani na kupambana na vikosi vya ulinzi kwa kwa takribani saa mbili. Akizungumzia tukio hilo leo katika uwanja wa Ihura, Ruto amesema watu hao walikuwa na lengo la kuvunja umoja na amani iliyojengeka ndani ya nchi hiyo. “Najua watu wengi mnafahamu kwamba jana nilikuwa na ugeni nyumbani kwangu, watu wema sana… lakini nataka kusema kwamba wanaodhani watavuruga umoja wetu au kuturudisha nyuma hawatafanikiwa,” alisema Ruto. “Natoa wito kwenu msiharibiwe na aina ya watu ambao wana lengo la kuvuruga maendeleo ya umoja wetu kama taifa,” aliongeza. Ruto na familia yake hawakuwa nyumbani wakati tukio hilo la uvamizi li...

Zitto: Serikali inadumaza kilimo..

Picha
Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo Chama cha ACT Wazalendo kimeiomba serikali  kutimiza ahadi yake ya kuwasaidia wananchi  wa Kusini pembejeo za kilimo ili kunusuru zao la korosho  ambalo kwa kiasi kikubwa linachangia pato la taifa. Katibu wa itikadi, mawasiliano ya umma na uenezi wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema serikali kupitia wizara ya kilimo  iliwaahidi wananchi wa Kusini kuwapatia pembejeo bure mwezi Mei mwaka huu katika kikao cha mwaka cha wadau wa korosho kilichofanyika mkoani Dodoma lakini ahadi hiyo haijatekelezwa hadi sasa. Shaibu amesema  baada ya serikali kutangaza kugawa  pembejeo bure,  baadhi ya vyama vya ushirika ambavyo vilikuwa vinanunua na kugawa pembejeo hizo  kwa wananchi vimelazimika kurudisha fedha kwa wanachi hao hali ambayo imeleta athari kwa wakulima hao ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya pembejeo kwa hivi sasa. Katika mapendekezo yake, chama hicho kimeitaka serikali kununua pembejeo zote na ...