Bastian Schweinsteiger amekubali kujiunga na Manchester United kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo atakuwa akivuna kitita cha pauni milioni 7.2 kwa mwaka. Schweinsteiger anajiandaa kusafiri kuelekea jijini Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na akifaulu zoezi hilo atasaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ya Old Trafford. Inaamika kuwa, uhusiano mzuri uliopo kati ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani na Louis van Gaal ilikuwa ni moja kati ya sababu zilizopelekea akubali ofa ya Manchester. Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild, Schweinsteiger, 30, ameshawataarifu mabosi wa Bayern kuhusu lengo lake la kutaka kujiunga na United na yuko mbioni kutua Manchester kukamilisha vipimo vya afya pamoja na kusaini mkataba mpya. Kilichobaki ni Manchester kukubaliana ada ya uhamisho na Bayern kwa ajili ya nyota huyo ambapo inasemekana vidume hivyo vya Ujerumani huenda vikahitaji dau la pauni milioni 15. SOURCE:(SHAFFIH DAUDA). ...