Lipumba asema yeye ndiye anayefaa kutawala
WAKATI kitendawili cha sitofahamu cha uwezekano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kusimamisha mgombea mmoja wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa , Profesa Ibrahim Lipumba, ameibuka na kusema taifa linahitaji kuwa na kiongozi mwenye uwezo wa kuinua na kuboresha uchumi kupitia sekta ya viwanda na kilimo.
Alisema uchumi unaosimamiwa na viwanda na sekta ya kilimo ndiyo njia pekee itakayowezesha kuongeza ajira nyingi za kada mbalimbali kwa vijana na uzalishaji mkubwa wa mazao kutawezesha kupatikana kwa malighafi ya viwanda na wananchi kupata lishe bora.
SOURCE:Habari Leo.
Maoni
Chapisha Maoni