Ndugai atoa ya moyoni kuhamia Dodoma..
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kitendo cha Serikali kuhamishia makao makuu Dodoma kitapunguza gharama kwa kuwa watumishi wake wote watakuwa mjini humo.
“Mwanzoni tulikuwa na gharama sababu iliwabidi watumishi waje kwa muda, lakini kadri tunavyoendelea tutaendelea kurekebisha,” amesema Ndugai akiwa ameambatana na mkewe baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma na kulakiwa na wabunge na watumishi wa Bunge.
“Uamuzi ni uamuzi tumeshapanga makao makuu ni Dodoma. Kwa hiyo suala la gharama linakuwa halina nguvu sana. Kama ulivyosikia mawaziri na makatibu wakuu wanataka kuja na hao ndiyo tunawahitaji sana kwenye vikao vyetu,” amesema.
Maoni
Chapisha Maoni