La Liga yaizidi makombe EPL..

FAINALI ya Kombe la UEFA Super Cup imemalizika usiku wa kuamkia jumatano, na kushuhudia Real Madid ikifanikiwa kuinyamazisha Sevilla baada ya kuichapa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Lerkendal Stadio nchini Norway.
Fainali ya Super Cup ilizikutanisha miamba ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, Real Madrid na Sevilla.
Kwa upande wao Sevilla ambao I mabingwa kombe la Shirikisho yaani Europa League kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Liverpool ya England.
RAMOS 93
Fainali ya mwaka huu imeshuhudia kwa mara nyingin Sergio Ramos akiisawazishia timu yake bao katika dakika za lala salama. Ramos alifunga bao la kusawazisha katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2014 baada ya Madrid kuwa nyuma kwa muda mrefu wa mchezo huku ikitarajiwa Atletico Madrid wangeibuka mabingwa wa Ligi ya Mabingwa.
Ramos alipachika bao hilo katika muda wa dakika 3 za nyongeza kabla ya mwamuzi kupiga filimbi ya kumaliza mchezo.
Katika fainali ya Ligi ya mabingwa mwaka 2016, Sergio Ramos alifunga bao la mapema kwa Real Madrid, lakini Atletico Madrid walisawazisha. Mwisho wa mchezo Real Madrid waliibuka wka ushindi wa matuta 5-3.
Fainali ya Super Cup, kwa mara nyingine Ramos alipachika bao katika dakika tatu za nyongeza na kusawazisha kuwa 2-2, yaani dakika ya 93. Kabla ya kuawaszisha bao hilo, ilidhaniwa Sevilla wangeibuka mabingwa. Ramos ni mzaliwa wa Sevilla na aliichezea klabu hiyo akiwa kinda.
LA LIGA VS EPL
Kufuatia ushindi huo wa Real Madrid umezidisha mpambano mkali kati ya Ligi Kuu ya Hispania yaani La Liga dhidi ya Ligi Kuu ya England maarufu kama EPL. Rekodi zifuazo zinaonyesha;
LIGI YA MABINGWA:
La Liga 10, EPL 4.
KOMBE LA SHIRKISHO
LA LIGA 8, EPL 2.
UEFA SUPER CUP:
La Liga 12, EPL 4
KLABU BINGWA DUNIA;
La Liga 6, EPL 2.
JUMLA
La Liga 36, EPL 12




Source:Tanzaniasports.com














































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..