Polisi wavunja mkutano wa CWT..


Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Dodoma uliolenga kuzungumzia ubadhirifu ndani ya chama hicho umevunjwa na polisi na wanachama kuamuriwa kutawanyika baada mwenyekiti wao, Samson Nkotya kukimbilia mahakamani kuuzuia.
Kwa mujibu wa walimu hao, mkutano huo uliitishwa na Katibu wa Chama wa Wilaya baada ya wajumbe wa mkutano mkuu zaidi ya nusu kuudai.
Mkutano huo ulikuwa na ajenda moja ya kujadili kusimamishwa kwa mweka hazina wa chama hicho bila ridhaa ya wanachama.
Hata hivyo, mkutano huo ulivunjwa muda mfupi baada ya Nkotya kukimbilia polisi akiwa na zuio la Mahakama ya Wilaya ya Dodoma lilitolewa juzi jioni.
Nkotya alipoulizwa alisema mkutano huo ulizuiliwa na Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, kupisha kesi ya msingi inayohusiana na uhalali wa mkutano huo.
“Mamlaka ya uamuzi wa mkutano mkuu wa wilaya yapo chini ya kamati ya utendaji ya wilaya na si chombo kingine chochote wala mtu mwingine yeyote,” alisema.
Katibu wa CWT Wilaya, Maswi  Rafael alisema mkutano huo umeitishwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na uliridhiwa na Katibu Mkuu CWT Taifa.“



Source:Mwananchi





















































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..