SERIKALI YAZIONDOA ZAIDI YA KAYA 30,000 ZISIZO NA SIFA KWENYE MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI.
Angela Kairuki Waziri wa nchi ofisi ya rais manejiment ya utumishi wa umma na utawala bora .
Serikali imeziondoa zaidi ya kaya elfu thelasini zisizo na sifa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na TASAF zikiwemo familia za watumishi wa serikali viongozi wa vijiji na watu wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi na kuwaingiza watu wasiyo na uwezo ambao waliachwa kwenye mpango huo.
Waziri wa nchi ofisi ya rais manejiment ya utumishi wa umma na utawala bora Angela Kairuki ametoa takwimu hiyo alipokuwa anazungumza na wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya wakurugenzi wa halmashauri na wadau wa maendeleo kutoka mkoa mitano kujadili mipango kazi na changamoto za TASAF.
Mkurugenzi mkuu wa TASAF Ladislaus Mwamanga amesema TASAF inaendelea na uhakiki wa kina kuhusu watendaji wanaohusika kuhujumu mipango ya tasaf na kueleza lengo la kikao hicho.
Source:Lindiyetu.com
Maoni
Chapisha Maoni