TTCL MATATANI KWA KUTOLIPA KODI YA MNARA KWA MMILIKI WA ARDHI...



Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeingia katika mgogoro na familia ya Mzee Akilimali Lutakwa (84) mkazi wa kijiji cha Ndelema wilayani Geita kutokana na kudai kutolipwa kodi ya huduma ya kila mwaka na kampuni hiyo ya mnara uliojengwa kwenye shamba lake tangu 2003.
Mzee huyo amesema kabla ya mnara huo kujengwa viongozi wa TTCL wilaya ya Geita na Mkoa wa Mwanza mwaka 2002 walifika nyumbani kwake kununua eneo la kujenga nyumba ya makazi lakini baadaye alishangazwa kuona unajengwa Mnara huo. 
Eneo hilo lenye ukubwa wa Robo heka linadaiwa kununuliwa na TTCL mwaka 2002 kwa laki 8 lakini tangu kujengwa kwa mnara huo Mzee Akilimali hajawahi kupokea kodi ya huduma ya kila mwaka. 
Watoto wa Mzee Akilimali, Majaliwa, Mapambano na Mashaka wanasema makubalinao ya kuuziana eneo hilo yalifanyika bila kujua kama kampuni hiyo inaenda kuwekeza mnara katika eneo hilo. 
Aidha, Mwenyekiti wa sasa wa kijiji hicho Baltazari Kitasigwa Mhoja amesema mnara huo hulipa Sh. 400,000 kila mwezi kwa ajili ya walinzi  na hakuna malipo mengine yanayofanyika na hata mzee huyo wakati anauza hakujua kama kuna uwekezaji wa Mnara.
Meneja wa TTCL Wilaya ya Geita Mohamed Sheikhe, amesema kuwa sio msemaji na kudai kuwa eneo hilo lilinunuliwa kwa mujibu wa sheria na tayari lina hati kutoka Idara ya Ardhi na hivyo ni mali halali ya kampuni na wala hawahusiki na kulipa kodi ya huduma kwa mzee huyo.



Source:Modewjiblog


































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..