Wakenya wazidi kumiminika Tanzania, wahofia machafuko...
Joto la uchaguzi nchini Kenya limezidi kupanda mara baada ya wananchi wengi wa nchi hiyo kuanza kumimika kuingia nchini Tanzania
Katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Horohoro uliopo mkoani Tanga, idadi ya Wakenya wanaovuka na kuingia Tanzania inazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda ikilinganishwa na siku zilizopita.
Baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa wamelazimika kuondoka nchini humo kwa hofu kuwa kuna uwezekano siku ya uchaguzi kukawa vurugu hivyo wameamua kujihami mapema.
“Tutakaa hapa mpaka pale uchaguzi utakapofanyika na mshindi kutangzwa, hali ikiwa shwari tutarudi, kwa sasa hali si shwari kabisa ndio maana unawaona Wakenya wengi wanazidi kukimbilia Tanzania,”amesema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Salehe
Hata hivyo, Afisa mmoja wa idara ya uhamiaji katika ofisi ya Horohoro ambaye hakutaka jina lake lijulikane, amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la abiria wanaoingia nchini kuliko wanaokwenda nchini Kenya.
SOURCE:Dar24
Maoni
Chapisha Maoni