Dawa na vipodozi vinavyoumua miili vyadaiwa sasa vinaingizwa kwa wingi katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Mamlaka ya chakula na dawa kanda ya nyanda za juu kusini imewatahadhalisha wananchi kuachana kabisa na matumizi ya dawa na vipodozi vinavyoumua sehemu za miili hususani makalio na maziwa kwa wanawake ambavyo vinaonekana kuanza kuingizwa kwa kasi na wafanyabiashara wasio waaminifu katika mikoa hiyo.
Meneja wa mamlaka ya chakula na Dawa, TFDA, Kanda ya nyanda za juu kusini,Roodney Alananga ametoa tahadhari hiyo kwa wananchi ambao wametembelea banda lake katika viwanja vya maonyesho ya kilimo nane nane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Baadhi ya wananchi wamekiri kuviona vipodozi hivyo sambamba na kushuhudia baadhi ya wanawake ambao tayari wamepata madhara kutokana na kutumia vipodozi hivyo.
Afisa wa forodha mkoani mbeya,Edward Amlle amesema kuwa mamlaka ya mapato,TRA,kama wasimamizi wa mizigo inaoingia na kutoka nchini,hawaruhusu wala kutoza ushuru katika bidhaa ambazo zimepigwa marufuku nchini hivyo vipodozi hivyo vitakuwa vinaingizwa nchini kwa njia za panya.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni