MAYWEATHER USO KWA USO NA BONDIA HUYU SEPTEMBER.

maywe

Hatimaye kile kitendawili cha nani atapigana na Floyd Mayweather September hii kimewekwa hadharani. Bondia Floyd Mayweather amemtangaza bondia Andre Berto kuwa ndiye mpinzani wake ifikapo September 12 mwaka huu.
Bondia Andre Berto ana asili ya Haiti na Marekani lakini pia amezua maswali mengi juu ya uwezo wake kwa Floyd Mayweather anayesaka rekodi ya ushindi wa 49 baada ya hadi sasa kuwa hajapoteza katika mapambano 48.
Andre Berto mwenye miaka 31 amepewa kipaumbele na The Money Team mbele ya mwingereza Amri Khan aliyehusishwa sana na pambano hili la Mayweather.
Khan ana rekodi nzuri ya 31-3 sanjari na KO 19 huku Andre Berto akipata matokeo ya 3-3 katika michezo yake mitatu ya mwisho.
Pambano hilo linatarajiwa kupigwa MGM Grand Arena mwezi September 12 mwaka huu huku kukiwa bado havitangazwa viingilio na dau baina ya wapiganaji.
Ikumbukwe kuwa Floyd Mayweather aliweka rekodi ya dunia ya mapato ya pambano la usiku mmoja walipopigana na Manny Pacquiao mei 2 na kuingiza dola 300m za kimarekani.
Wengi wanasubiri kuona pambano hili la The Best Ever linaingiza mtonyo kiasi gani hapo September 12, huku pia ikisubiriwa huenda likawa pambano la mwisho ama la kwa mkongwe Floyd Mayweather.
SOURCE:Shaffihdauda.com








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...