Mkwasa kawaita mastaa hawa 29 kuunda Kikosi cha Taifa Stars kitakachopaa kwenda Uturuki..
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaongia kambini Jumapili katika hoteli ya Tansoma kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.
Katika kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, ambao baadaye watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015.
Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi Jijini Istanbul, Uturuki ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.
Wachezaji watakaongia kambini Jumapili ni makipa, Ally Mustafa ‘Barthez’ wa Yanga SCna Aishi Manula wa Azam FC.
Mabeki ni Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul,Mwinyi Haji (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ naKelvin Yondani (Yanga SC).
Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Telela(Yanga SC), Abdi Banda na Said Ndemla wote wa Simba SC… Mawinga ni Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Simon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano na Farid Mussa (Azam FC), wakati washambuliaji ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji wanaocheza nje waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DRC), Mrisho Ngassa (Free State – Afrika Kusini) naHassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – England).
SOURCE:Millardayo.com
Maoni
Chapisha Maoni