WATUHUMIWA WAPEWA ADHABU YA KUNUNUA JEZI ZA BAYERN MUNICH..
Hakimu Jung amemaliza kesi ambayo iliyokua mezani kwake kwa style ya pekee ambayo imempa umaarufu sana kwenye magazeti ya huko Ujerumani. Hakimu huyo alikua na kesi ya mashabiki wawili wa 1860 Munich ambao walimfanyia fujo shabiki mmoja wa Bayern Munich kwenye kituo cha treni.
Shabiki huyo alifungua mashtaka na mashabiki wa 1860 Munich walipandishwa kizimbani na kukutwa na kosa hilo. Badala ya kuwapeleka jela miezi 15 kama sheria inavyosema, hakimu huyo mwanamke aliwapa adhabu ya kwenda kufanya shopping ya full kit kwenye duka la Bayern Munich pamoja skafu.
Kila pea moja iliwa-cost Euro 100 na pia waliambiwa wamlipe Euro 500 shabiki huyo wa Bayern Munich kila mtu kwa ajili ya maumivu waliyomsababishia. Alipoulizwa kwanini ametoa adhabu ya aina hiyo, jaji Jung alisema kwasababu ugomvi huo ulitokana na chuki za kishabiki dhidi ya club ya Bayern Munich. Hivyo basi kuwalazimisha wafanye shopping kwenye maduka ya Bayern ambapo watakua wanaichangia maendeleo ya club hiyo, itakua ina waumiza zaidi.
SOURCE:Shaffihdauda.com
Maoni
Chapisha Maoni