MALI: HOTELI YASHAMBULIWA KATIKA MJI WA SEVARE...



WATU waliojihami kwa kutumia bunduki wameshambulia zaidi ya hoteli mbili katika mji wa Sevare eneo la katikati ya nchini Mali.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kwamba watu hao waliokuwa  wakiendesha pikipiki wameingia katika eneo hilo na kuanza kufyatua risasi kwenye majengo hayo.
Imebainika kwamba ingawa Mji wa Sevare una kituo cha jeshi la anga pamoja na wanajeshi kadhaa wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani lakini bado matatizo kama hayo hujitokeza.

SOURCE:Efm radio

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...