Tanzania bado hali tete katika viwango vya FIFA imeshuka hadi nafasi hii..

Shirikisho la Soka ulimwenguni FIFA huwa na utaratibu wa kutangaza viwango vya soka vya nchi wanachama kila mwezi lakini Tanzania imeonekana kuzidi kushuka, ndani ya kipindi cha miezi  miwili imeshuka kwa nafasi 13 hii inatokana na matokeo mabovu kwa mechi za Taifa Stars za hivi karibuni.
TFF1
Tanzania mwezi uliopita iliporomoka hadi nafasi ya 139 na mwezi huu imeshuka tena hadi nafasi ya 140 ikiwa imeshuka kwa nafasi moja tena. Licha ya  TFF kumfukuza kochaMart Nooj kufuatia mwenendo wa matokeo mabovu na nafasi yake kuchukuliwa na kochaCharles Mkwasa lakini bado haijawa suluhu ya Stars kupata matokeo mazuri.

malinzi
Stars imekuwa na matokeo mabovu kwa mechi za hivi karibuni kwani ilifungwa mechi zake zote tatu za kundi B katika michuano ya COSAFA ambapo Tanzania ilishiriki kama timu mwalikwa, mechi ya kwanza kufuzu AFCON ilifungwa goli 3-0 na Misri baada ya hapo ikatolewa na Uganda kufuzu michuano ya CHAN 2016 kwa jumla ya goli  4-1.

SOURCE:Millardayo.com















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...