HIVI NI VITU VINAVYOUPA UGUMU MCHEZO WA SIMBA VS MGAMBO JKT UWANJA WA MKWAKWANI..

Peter Mwalyanzi (kulia) wa Simba kipambana na Ayub Masoud wa African Sports wakati timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Mkwakwani kwenye mchezo wao wa uunguzi wa VPL msimu huu
Peter Mwalyanzi (kulia) wa Simba kipambana na Ayub Masoud wa African Sports wakati timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Mkwakwani kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa VPL msimu huu.

Simba Sports Club leo inashuka kuwakabili maafande wa Mgambo JKT kutoka wilaya ya Handeni kikosi cha 835 JKT Kabuku jijini Tanga mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jioni ya leo.
Kuelekea mchezo huo, mtandao huu umekuletea baadhi ya vitu muhimu vinavyoupa ugumu mchezo huo.
Historia ya timu hizo kweye uwanja wa Mkwakwani
Simba imeshindwa kutamba kwenye uwanja wa Mkwakwani mbele ya Mgambo JKT kwa kipindi cha misimu miwili sasa, ushindi pekee kwa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam ikiwa kwenye uwanja wa huo umekuwa ni sare.
Matokeo ya mechi za ufunguzi wa ligi msimu huu
Simba
Mnyama aliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya African Sports kwenye uwanja wa Mkwakwani uwanja ambao umekuwa ukiitesa Simba kupata ushindi dhidi ya timu za mkoani humo ikiwa ilishindwa kuibuka na ushindi kwa misimu miwili mfululizo dhidi ya klabu za Coastal Union na Mgambo JKT kabla ya kushinda mbele ya African Sports mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mgambo JKT
Wao waliambulia sare ya kufungana goli 1-1 na timu ya Ndanda FC ya mkoni Mtwara kwenye mchezo wao wa ufungui wa ligi msimu huu uliochezwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mechi ya mwisho timu hizo kukutana kwenye uwanja wa Mkwakwani
Mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Simba ilichezea kichapo cha goli2-0 mbele ya Mgambo JKT.
Maandalizi ya timu zote kuelekea mchezo wao wa leo
Simba
Wameendelea na mazoezi yao kwa siku zote ambazo wamekuwa jijini Tanga wakifanya mazoezi yao kwenye uwanja wa Disuza, lakini jana wakafanya mazoezi yao ya mwisho kwenye uwanja wa Mkwakwani uwanja ambao utatumika kwa mchezo wao dhidi ya Mgambo JTK.
Mgambo JKT
Kikosi hiki chenyewe kilijichimbia kwenye kambi ya kikosi cha wanamaji pembezoni kidogo mwa jiji la Tanga kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa leo.
Wasemavyo makocha/nahodha wa timu hizo
Simba
Nahodha wa timu hiyo Musa Hassan Mgosi amesema kuwa, timu iko vizuri na morali kwa wachezaji ipo juu na wanazitaka pointi tatu kwa nguvu zote.
Mgambo JKT
Bakari Shime ‘mchawi mweusi’ kocha wa Mgambo JKT amesema amekiandaa kikoi chake kwa michezo 30 na mchezo wa leo ni miongoni mwa michezo hiyo. Ameweka wazi pia kuwa atautumia vyema uwanja wake wa nyumbani kama silaha yake kuituliza Simba.


SOURCE:Shaffihdauda.com


















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...