WAZIRI AWAASA VIJANA KUPAMBANA MICHUANO YA AIRTEL..

Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiongea wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel  Rising Stars katika ngazi ya taifa

Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiongea wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars katika ngazi ya taifa.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara amewaasa vijana wanaoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars kwa vijana chini ya miaka 17, kupambana kwa bidii ili kufanikisha malengo yao.
Dr. Mukangara alisema hayo wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mukangara,  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema kuwa Dr. Mukangara amemimina pongezi za dhati kwa kampuni ya Airtel hapa nchini kwa kuendelea kutoa sapoti kwa maendeleo ya soka hapa nchini ili kuitangaza Tanzania kimataifa.
“Angalieni timu ya taifa ya wasichana-Twiga Stars. Kuna wachezaji wengi sana ambao wametokana na michuano hii” , alisema huku akilitaka Shirikisho la Soka nchini (TFF) na wadau wengine kutumia michuano hii kutafuta vipaji vipya kwa maendeleo ya soka hapa nchini.
Alisema kuwa kwa kuweka msisitizo mkubwa kwenye soka la vijana, Tanzania itakuja kuwa moja ya nchi zenye nguvu kubwa katika soka. “Mataifa yote yenye nguvu katika soka duniani, yamefanikiwa kutokana na programu hizi”, alisema.
“Kiwango chetu cha soka kitakapoimarika, tutakuwa na fursa nzuri sana ya kujitangaza kimataifa hasa vivutio vyetu kama vile Mlima Kilimanjaro ambao ndio mrefu kuliko yote duniani na hifadhi zetu za taifa. Hii itafanya watalii wengi kuja hapa nchini hivyo kuongeza pato la taifa”, alisema
Pia aliwashauri vijana kuongeza juhudi zaidi kwani mchezo wa soka kwa sasa umekuwa ni moja ni sekta rasmi ambayo inatoa ajira  kwa kiasi kikubwa, hivyo juhudi zao ndio msingi wa mafanikio yao na familia zao.
Akizungumza katika hafla hiyo hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel nchini, Beatrice Singano Mallya, alisisitiza kampuni yake kuendelea kudhamini michuano hiyo huku akionesha kuridhishwa na jinsi Wizara husika, TFF na wadau wengine wanavyotoa sapoti kubwa sana kwa kampuni hiyo. “Tunajivunia sana mafanikio yaliyopatikana kupitia michuano hii na tunaahidi kuendelea kutoa sapoti kama ambavyo tumekuwa tukifanya”, alisema.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya karume jijini Dar es Saalam



















Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya karume jijini Dar es Saalam.
Kwa upande wake, makamu wa rasi wa TFF Wallace Karia aliwashukuru Airtel na kuyaomba makampuni mengine kuiga mfano huu. Sherehe za ufunguzi zilitanguliwa na michezo miwili, ambapo wenyeji-timu ya wasichana ya Temeke iliwatungua bila huruma Arusha kwa magoli 8-0, kabla ya hapo baadaye Mwanza kuifunga Kinondoni kwa bao 1-0, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja huo huo wa Karume.
Mwanamuziki wa Hip Hop Nay Wa Mitego akitumbuiza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa Hip Hop Nay Wa Mitego akitumbuiza wakati wa ufunguzi wamashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.



SOURCE:Shaffihdauda.com






















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...