Serikali ya Kenya yalaumiwa kufanya ukiukaji wa haki za binadamu...

Kenya polisi wakifanya doria mbele ya Msikiti wa Musa mjini Mombasa huko Kenya
Kenya polisi wakifanya doria mbele ya Msikiti wa Musa mjini Mombasa huko Kenya


Tume ya taifa ya haki za binadamu nchini Kenya inawashutumu polisi na majeshi ya usalama kwa ukiukaji mbali mbali ikiwemo mauaji na mateso katika mapambano  yanayoendelea dhidi ya ugaidi nchini humo.
Tume ilisema katika ripoti mpya ya Jumanne kwamba ukiukaji wa haki za binadamu umesambaa na uliratibiwa  vyema. Wachunguzi wanasema waliambiwa kwenye kesi mbali mbali za washukiwa kwamba walikamatwa kiholela na kuwekwa jela kuanzia  saa kadhaa hadi siku nyingi katika hali ya msongamano mkubwa na hali duni.
Polisi wa Kenya na harakati za msako wa magaidi





Polisi wa Kenya na harakati za msako wa magaidi.
Kuna shutuma za mateso, kupigwa, kumwagiwa maji na kuchomwa na  nyaya za umeme. Baadhi ya washukiwa walining’inizwa kwenye miti na wengine waliachwa  wakang’atwe  na wadudu.
Ripoti hiyo ilisema watu wenye asili ya kisomali na waislam wamekuwa walengwa wakubwa. Familia zinatafuta taarifa juu ya kupotea kwa jamaa zao na wanapata msaada kidogo kutoka kwa maafisa.
Tume hiyo ilisema huku ikitambua changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Kenya katika kupambana na msimamo mkali  na ugaidi, lazima hilo lifanyike kisheria  na kulingana na viwango vinavyokubalika ulimwenguni vya haki za binadamu.
Maafisa wa Kenya bado hawajajibu lolote juu ya ripoti hiyo.    

SOURCE:VOA


























Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...