‘Tumieni takataka kutengeneza bidhaa’..



Dar es Salaam. Watanzania wametakiwa kutumia takataka zinazozagaa mitaani kutengeneza bidhaa zenye thamani na ubora kibiashara.
Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya Archipelago, Sarah Scott alisema hayo jana na kuongeza kuwa ufukwe wa Msasani umeathirika zaidi na uchafuzi wa mazingira.
“Tunaweza kujiinua kiuchumi kutokana na takataka mbalimbali na tukafanikiwa sana. Hii itabadilisha sana hisia za watu juu ya uchafu na tutaleta maendeleo kwa uchumi.
“Inapaswa kufikiria sana jinsi ya kuwa wabunifu na kutengeneza bidhaa nzuri kwa ajili ya kuuza nchini au kusafirisha nje ya nchi na kuweza kuingiza fedha za kigeni,” alisema.
Ofisa wa Kampuni ya Resegla inayonunua takataka, Philip Steven alisema taka zinaweza kuongezwa thamani badala ya kuonekana kama uchafu katika mazingira ikiwa zitatunzwa vizuri.
“Watumiaji wanapomaliza matumizi yao na kubakisha vitu ambavyo tunaita takataka, huwa hawavitunzi vizuri.
“Mfano chupa haitakiwi kuwa na michanga, unapopeleka karatasi kiwandani isiwe imelowa, hivyo ni vitu ambavyo watu wanatakiwa kuvifahamu,” alisema Steven.
SOURCE:Mwananchi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...