Wananchi wadai itungwe sheria ya kuwabana viongozi wadanganyifu...


Baadhi ya wananchi wa mkoa wa shinyanga wameiomba serikali kuunda sheria itakayowabana viongozi ambao watashindwa kutekeleza ahadi zao walizoziahidi wakati wa kampeni za kuomba kura kwakuwa wengi wao wamekuwa wakitoa ahadi zisizotekelezeka hali ambayo imekua ikidumaza shughuli za maendeleo na kusababisha kutokukua kiuchumi.

Wakitoa malalamiko yao baadhi ya wananchi wa mji wa Shinyan.ga wamesema wanashangaa kuona wakati wa uchaguzi wagombea wakiahidi ahadi nyingi zinazoleta matumaini lakini punde tu kiongozi anapoingia madarakani ahadi hizo zinayeyuka na kuwaacha wakiendelea kuteseka kwa kipindi chote cha miaka mitano huku baadhi ya vijana wakiitaka halmashauri ya manispaa isitumike vibaya na baadhi ya vyama vya siasa.
 
Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya kambarage mjini Shinyanga Bw.Hasan Mwendapole amewataka wananchi kuchuja wagombea kwa kutathmini utekelezaji wa sera na ilani ya vyama vyao huku akiahidi kuwa kipaumbele chake cha kwanza atakapopata ridhaa ni kuboresha elimu na kuinua uchumi wa vijana.


SOURCE:ITV



















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...