Navy Kenzo gumzo Nigeria...

Navy Kenzo

KUNDI la Navy Kenzo linaloundwa na wapenzi, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ na Aika Mareale ‘Aika’ limekuwa gumzo nchini Nigeria kutokana na wimbo wao wa ‘Game’ waliomshirikisha Vanessa Mdee kupigwa mara kwa mara katika redio na televisheni za huko.
Nahreel alisema amekuwa akipokea simu kutoka kwa watangazaji wa vituo mbalimbali vya redio na runinga vya nchini humo kwa ajili ya mahojiano, huku wengine wakimpongeza kwa wimbo huo unaofanya vizuri nchini humo.
“Wanadai ‘audio’ na video ya wimbo wetu unafanya vizuri nchini mwao, ndiyo maana upo katika chati za juu katika vituo vya redio na runinga nchini humo, tunashukuru na tutazidi kuandaa kazi nzuri kama inavyoendelea kujitokeza kwa kuvuka malengo ya tulivyojipangia kimafanikio ya kazi zetu,’’ alieleza Nahreel.

SOURCE:Mtanzania





















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...