LIONEL MESSI ATAFIKISHA MECHI 100 KWENYE MECHI INAYOFUATA YA UEFA…HII NI HISTORIA YAKE KWENYE UEFA...

1906132

Kwa mara ya kwanza Lionel Messi aligusa mpira wa UEFA champions league kwenye mashindano rasmi ilikua ni mwaka 2004 ambapo alicheza kwenye kikosi cha Barcelona dhidi ya Shakhtar Donetsk.
Goli lake la kwanza alifunga akiwa kwenye mechi dhidi ya Panathinaikos kwenye group stage mwezi November mwaka 2005 na Barcelona walishinda mashindano yake.
Akiwa chini ya Pep Guardiola mwaka 2008-09, Messi alianza kufanya vizuri baada ya kufunga magoli 12 kwenye mechi muhimu hasa kwenye fainali ambayo Barcelona waliifunga Manchester United kwenye fainali huko Rome ndani ya uwanja wa Stadio Olimpico, uwanja huo ndio hapohapo Messi atacheza kufikisha mechi 100.
Mwaka 2011-12 Messi aliweka rekodi ya kufunga magoli ambapo alifunga mara 14 akicheza mechi 11. Hizi ni rekodi chache na matukio ambayo Lionel Messi ameyafanya kwenye UEFA Champions League na anategemewa kuendelea kama alivyofanya kwenye msimu uliopita.

SOURCE:Shaffihdauda.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Imetangazwa noti yenye muonekano mzuri kuliko zote duniani kwa mwaka 2016..

Picha 10 za Ikulu zilizo nzuri zaidi Duniani...