Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2016

Trump asisitiza kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji..

Picha
Donald Trump amesema kuwa atajenga ukuta kuwazuia wahamiaji kutoka Mexico Mgombea urais wa chama cha Rupublican nchini Marekani Donald Trump amesema kuwa atabuni mfumo ambao utasaidia serikali kudhibiti uhamiaji. Akizungumza wakati wa kampeni katika jimbo la Iowa bwana Trump alisema kuwa mfumo huo utasaidia kuwatimua watu ambao wanaishi nchini Marekani licha ya muda wa visa zao kumalizika. Pia alirejelea wito wake wa kujengwa ukuta kati ya mpaka wake na Mexico kuwazuia wahamiaji. Source:BBC

Aliyetuhumiwa na kashfa ya kuuza tiketi Rio aachiliwa huru..

Picha
Mshukiwa wa kashfa ya uuzaji tiketi katika michezo ya Olimpiki ya Rio Kevin Mallon Wakuu wa Brazil wamemtoa gerezani mfanyibiashara wa Ireland, aliyeshukiwa kuhusika na kashfa kuhusu uuzaji wa tikiti za Michezo ya Olimpiki iliyofanywa Rio. Kevin Mallon, mkurugenzi wa kampuni moja ya takrima ya Uingereza, THG, alizuiliwa kwa siku tatu kwenye gereza lenye ulinzi mkali mjini Rio. Alikamatwa akiwa na mamia ya tikiti, zilizokusudiwa Halmashauri ya Olimpiki ya Ireland ambapo baadhi ya tikiti zilikuwa za sherehe za ufunguzi na ufungaji wa michezo hiyo. Kampuni ya THG imekanusha kuwa ilifanya kosa. Wakili wa bwana Mallon, alisema kufunguliwa kwa mteja wake, hakuathiri kesi ya mtu mwengine aliyeko kizuizini kwa sababu ya kashfa kuhusu tikiti, Patrick Hickey ambaye ni mkuu wa halmashauri ya Olimpiki ya Ireland. Source:BBC ...

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NCHINI SWAZILAND,KUMUWAKILISHA RAIS MKUTANO WA 36 WA SADC (+PICHAZ)

Picha
PICHA NYINGINE Source:Michuzi Blog

Mkutano wa maendeleo kati ya Japan na bara la Afrika wakamilika jijini Nairobi.

Picha
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe akiwa na viongozi wa Afrika wakati wa mkutano wa TICAD jijini Nairobi nchini Kenya Agosti 27, 2016. Mkutano wa siku mbili wa Maendeleo kati ya serikali ya Japan na bara la Afrika (TICAD) umemalizika siku ya Jumapili jijini Nairobi nchini Kenya. Huu ulikuwa ni mkutano wa sita kati ya Japan na viongozi wa Afrika, na kufanyika mara ya kwanza barani Afrika kujadili maswala ya ushirikiano wa kuinua uchumi na biashara. Wakati wa mkutano huu, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alitangaza kuwa serikali yake itatoa Dola za Marekani Bilioni 30 kusaidia mataifa ya Afrika kujenga na kukarabati miundo mbinu, kama barabara, bandari na vituo vya kuzalisha umeme ikiwa ni pamoja na kuimarisha sekta ya elimu na afya. Japan itatuma fedha hizo kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika, kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kufanikisha maendeleo hayo. Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe (Kushoto) akisalimiana na rais wa Chad na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati wa M...

Polisi watibua ndoa ya wapenzi wa jinsia moja Nigeria..

Picha
Wapenzi wa jinsia moja. Maafisa wa polisi nchini Nigeria wanawasaka watu wawili wanaotuhumiwa kwa kuandaa ndoa ya wapenzi wa jinsia moja katika mji wa kaskazini wa Nigeria wa Sokoto,msemaji wa polisi ameiambia BBC. Mmiliki wa nyumba ambayo sherehe hiyo ilifanyika wikendi iliopita amekamatwa lakini washukiwa wakuu bado hawajapatikana. Mapenzi ya jinsia moja nchini Nigeria ni kinyume na sheria. ''Polisi wameanzisha uchunguzi mkali kwa lengo la kuwafungulia mashtaka watu hao wawili kwa kuhusika katika tendo linalokiuka maumbile'',aliongezea. Watu wengine waliokuwa katika sherehe hiyo walitawanyika wakati polisi walipowasili katika eneo la sherehe hiyo. Source:BBC ...

RIPOTI MAALUM YA MKUTANO WA DHARURA ULIORIDHIA KUIKODISHA YANGA KWA MANJI..

RASIMU ZA DONDOO YA MKUTANO WA DHARURA WA MWAKA WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB AGOSTI 6, 2016. SALA ZA UFUNGUZI Sala ya Wakristo ilisomwa. Sala ya Waislam ilisomwa. UFUNGUZI WA MKUTANO ULIFANYWA NA  MWENYEKITI, WA young africans sports club SAA 5 ASubuhi. kupitishwa kwa ajenda kulitolewa na  Mwenyekiti, WA YOUNG africans sports club SAA 5:30 ASUBUHI. Wanachama walikubaliana kuipitisha Ajenda. MASUALA YA SOKA – yalisomwa na  Mwenyekiti, wa young africans sports club. Msimu uliopita, Klabu: Ilipata ushindi wa Ngao ya Jamii; Ilikuwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015 /2016 Vodacom; Ilikuwa mshindi wa Kwanza wa Kombe la FA; Ilifikia raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa na ikapoteza mchezo wa marudiano nchini Misri; na Ilifikia hatua ya Kombe la Shirikisho na Hatua ya Makundi baada ya karibu miaka 20 kupita bila kufikia hatua hiyo ya makundi ya Mashindano ya Kimataifa ya Bara la Afrika. Wakati Klabu ya Young Africans Sports ni klabu pekee ambayo inaiw...